DC CHONJO AWATAKA WANANCHI KUCHUKUA TAHADHARI YA UGONJWA WA CORONA.
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Regina Chonjo akizungumza na Wadau kuhusu tahadahri ya Ugonjwa wa Ukimwi. |
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba, akizungumza na Wadau mbalimbali juu ya hatua ambazo Manispaa imezichukua katika kujikinga na Corona. |
Mganga Mkuu wa Manispaa ya Morogoro, Dr Ikaji Rashidi, akitoa taarifa na kuwapatia elimu wadau waliohudhuria katika mkuatano wa kujadili kwa pamoja ugonjwa wa Corona. |
Afisa Afya Manispaa ya Morogoro, Prisca Gallet, akionyesha mfano wa jinsi ya kunawa na sabuni kama moja ya kinga ya virusi vya Corona. |
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba, akitoa maelekezo kwa wajumbe waliohudhuria katika mkutano wa kujadili kwa pamoja jinsi ya kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona. |
Wakuu wa Idara , Manispaa ya Morogoro, wakifuatilia kwa umakini mjadala wa wadau mbalimblai juu ya kujikinga na ugonjwa wa Corona. |
Wakuu wa Idara , Manispaa ya Morogoro, wakifuatilia kwa umakini mjadala wa wadau mbalimblai juu ya kujikinga na ugonjwa wa Corona. |
Mganga Mkuu wa Manispaa ya Morogoro, Dr. Ikaji Rashidi, akitoa maelekezo kwa wajumbe waliohudhuria katika mkutano wa kujadili kwa pamoja jinsi ya kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona. |
Mwananchi akitoa ushauri jinsi ya kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona. |
MKUU wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Regina Chonjo, amewataka wananchi kuchukua tahadhari na
ugonjwa wa corona kabla ya ugonjwa huo haujaanza kuingia katika Wilaya hiyo.
Akizungumza leo katika Ukumbi wa Manispaa ya Morogoro Machi 17, 2020 akiwa na wadau mbalimbali ambapo amesema kuwa wananchi wanatakiwa kuacha kusalimiana kwa kushikana mikono ili kujikinga na Corona
Amesema kila mwananchi ahakikishe ana nawa mikono na maji tiririka na sabuni ikiwa ni miongoni mwa hatua za awali za kujikinga.
Pia ameagiza Maafisa Tarafa wote Wilaya ya Morogoro kuchukua
taarifa kwa Watendaji wa Kata ili kuangalia hali za afya za wananchi na kuweza
kubaini kama yupo atakayekutwa na maambukizi hayo kwa ajili ya matibabu.
Hata hivyo amezitaka Mamlaka zote zenye kusimamia vifaa Tiba
zihakikishe kwamba zinaweka usimamizi mzuri wa upatikanaji wa vifaa hivyo kwa uharaka na bei nafuu ili wananchi
waweze kuchukua tahadhari ya ugonjwa huo.
Aidha, amezitaka Ofisi zote za Serikali na binafsi kuweka mikakati
maalumu ya kuzuia ugonjwa huo huku kila Ofisi ikiweka Maji pamoja na sabuni nje
ili kila anayetaka huduma lazima anawe na kuweza kupatiwa huduma.
Amesema kuhusu suala la utoaji wa elimu kwamba ipo Timu ya
Wataalamu inayopita katika Taasisi mbalimbali ikiwemo Shuleni, Viwandani,
Vyuoni, Sokoni pamoja na Stendi za mabasi na sehemu zote zenye mkusanyiko.
“Tumeitana hapa kwa ajili ya kutoa tahadhari ya ugonjwa huu,
ningeomba kila mmoja wetu awe balozi wa mwenzake, tahadhari kama Serikali
tumeshachukua, kilichobakia ni sisi wananchi tupeane zaidi elimu jinsi ya
kujikinga japo Wilaya yetu ipo salama, hata katika Mabenki tutawapelekea barua
wahakikishe ATM zao wanaweka Vifaa vya kutakasa mikono hii ni lazima, pia
ukiwa unapiga chafya weka kitambaa au kiwiko chako cha mkono puani ili usiwalushie
vitone vya mate wenzako, tuwe wasafi
tukirudi nyumbani kwetu tunawe maji na sabuni ili tusiambukize na wenzetu
waliopo majumbani,”Amesema DC Chonjo.
Naye Mganga Mkuu wa Manispaa ya Morogoro, Dr. Ikaji Rashidi, amesema tayari wametenga eneo la kituo Kata ya Mkundi lenye wodi mbili ya kike na wanaume katika eneo lilitengwa kwa ajili ya Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ili eneo hilo litumike u kwa ajili ya wagonjwa watakaopatikana na corona ndani ya Wilaya hiyo na mazingira pamoja na vifaa vyote vipo tayari .
Naye Mganga Mkuu wa Manispaa ya Morogoro, Dr. Ikaji Rashidi, amesema tayari wametenga eneo la kituo Kata ya Mkundi lenye wodi mbili ya kike na wanaume katika eneo lilitengwa kwa ajili ya Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ili eneo hilo litumike u kwa ajili ya wagonjwa watakaopatikana na corona ndani ya Wilaya hiyo na mazingira pamoja na vifaa vyote vipo tayari .
“’Leo tupo hapa , kila mmoja wetu akitoka hapa awe balozi wa
mwenzake kwani janga hili japo halijafika katika Manispaa yetu lakini kinga ni
bora sana , na kama kuna mtu ana dalili ya ugonjwa huo asiende kutoa taarifa
kituo cha afya anatakiwa apige simu kwa mtoa huduma ili aweze kuhudumiwa na
kuweka kuwa tahadhari ya kuwaambukiza wengine" Amesema Dr. Ikaji
Kuhusu ugonjwa huo kuwapata sana Wazee, Dr Ikaji amesema
takwimu zinaonyesha asilimia kubwa ya watu wanaokufa kutokana na ugonjwa huo ni Wazee pamoja na wagonjwa wenye ugonjwa wa muda mrefu kwani wao wana kinga ndogo sana
ya mwili.
Sambamba na Hilo , Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro , Sheilla Lukuba, amesema wanatarajia kuagiza vipima joto mwili ambavyo vitasaidia kupima joto kwa mbali hususani kwenye maeneo mbali mbali na kuwatoa hofu wananchi kwamba Manispaa imejipanga kutoa elimu na kufanya matangazo yenye kuelimisha huku hatua mbalimbali zikiwa tayari zimeshachukuliwa na Timu ya Wataalamu wa afya .
Kwa upande wa miongoni mwa wachangiaji maada, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Steven Mashishanga,
ameiomba Serikali kuangalia kwa jicho la tatu uwezekano wa kuweka bei elekezi
na nafuu ya dawa au vifaa vitakavyotumika kujikinga na Ugonjwa wa Corona kwa kuzingatia kipato cha wananchi wa hali ya
chini.
Amesema kumekuwa na tabia baadhi ya watu wanapoona janga
limeingia nchini wamekuwa wakipandisha bei dawa na kufanya kama njia ya
kujiongezea kipoto badala ya kuuza kwa bei nafuu ili kila Mtanzania aweze
kumudu gharama za dawa.
Post a Comment