SCANIA IKO TAYARI KULETA MABASI YANAYOTUMIA GESI YA ASILI NCHINI TANZANIA
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya magari ya Scania Tanzania Ltd, Lars Eklund, akizungumza wakakati wa kampuni hiyo kutangaza kuleta mabasi yatumiayo gesi asilia ambayo ni bora kwa soko la Tanzania hasa kwa usafiri wa umma (Bus RapidTransit) hafla hiyo imefanyika leo katika ofisi kuu ya Scsnia iliyoko vingunguti jijini Dar es Salaam. Mwengine pichani ni Meneja Masoko wa Scania, Eliavera Timoth. hafla hiyo imefanyika leo katika ofisi kuu ya Scania iliyoko vingunguti jijini Dar es Salaam. |
Kampuni ya magari ya Scania Tanzania Ltd yatangaza kuleta mabasi yatumiayo gesi
asilia ambayo ni bora kwa soko la Tanzania hasa kwa usafiri wa umma (Bus Rapid
Transit). Bidhaa hii ni sehemu ya juhudi ya kampuni kuhakikisha inaongoza
katika kuboresha sekta ya usafirishaji nchini. Kampuni ya Scania inaamini kuwa
ni wakati sahihi kwa Tanzania kuingiza katika mfumo huu na mingine kwa ajili ya
kuboresha maisha ya watu kimazingira na kiuchumi.
Tanzania
ina akiba kubwa ya gesi asilia na inahitaji maelfu ya mabasi ya jiji kwa mfumo
wa BRT ambayo kampuni ya Scania inaweza kuleta. Kampuni ya Scania imekuwa
imefanikiwa kuleta magari ya mfumo wa gesi kwa muda mrefu sehemu mbalimbali
duniani kama Amerika Kusini, Ulaya na Australia.
Moja
ya faida ya mabasi yanayoendeshwa na mfumo wa gesi asilia (Compressed Natural
Gas) ni kwamba mfumo wake wa injini utasaidia kupunguza hewa chafu (Carbon
dioxide) kwa asilimia 20 ambapo CO2 inatajwa kuwa ndio chanzo cha joto kali
duniani, itapunguza gharama za uendeshaji, gharama kwa abairia na itasaidia
serikali kuongeza mapato kupitia uuzaji wa gesi asilia.
Akizungumza
na wanahabari katika ofisi kuu iliyoko Vingunguti kando na barabara ya Julius
Nyerere jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Scania Tanzania, Lars
Eklund amesema Tanzania inaelekea kuwa nchi ya viwanda, hivyo ufanisi
unahitajika na kwamba mazingira yasisahaulike.
“Tunaamini
ya kwamba Tanzania inahitaji kuwa na teknolojia mpya ili iendane na kasi ya
nchi zilizoendelea. Tanzania ni tajiri sana kwa gesi asilia na ni muhimu
kutumia nishati hii ya ndani kwa faida ya nchi, nchi itapata faida sana kwani
itapunguza kiasi cha mafuta yanayoagizwa nje” na badala yake inaweza kuuza gesi
ya ndani kwa waendeshaji wa ndani. Hakuna njia bora na ni ghari sana kujaribu
kubadili injini ya dizel kuwa injini ya gesi. Alisema Bwana Lars Eklund.
Kumekuwa
na taaria kupitia vyombo vya habari kutaka kubadili mfumo wa sasa wa magari ya
BRT kutoka injini ya dizel kwenda injini ya gesi, suala hili halina tija
kiufundi na kiuchumi kwa sababu injini ya dizeli imeundwa kufanya kazi katika
mzunguko wa dizeli wakati injini za gesi na petrol zinaendeshwa kulingana na
kanuni ya Otto na ujazo wa kuziba cheche. Kwa hiyo ni muhimu sana kuwepo kwa
mipango bora ya upanuzi wa miundo mbinu ya gesi asili ambapo itasaida wauzaji
na waendeshaji kuthubutu kuwekeza katika bidhaa sahihi za gesi asilia
zitakazotumiwa barabarani haraka iwezekanavyo. Alisema Bwana Lars Eklund.
Kama
sehemu ya kukuza huduma zake nchini, kampuni ya Scania Tanzania inatafuta
kushirikiana na taasisi mbalimbali za elimu kufadhili wanafunzi wanaochukua
elimu kuhusu matumizi ya gesi asilia (Compressed Natural Gas). Hii itasaidia
kuongezeka kwa idadi ya mafundi na wataalamu katika uwanja huo hivyo kuongezeka
kwa msaada kwa watumiaji wa mabasi yenye mfumo wa gesi nchini. Mpango huu sio
tu sehemu ya kujitolea kuboresha huduma lakini pia ni njia ya kurudisha fadhila
kwa jamii zetu zinazotuzunguka. Alisema Bwana Eliavera Timoth, Meneja Masoko
Scania Tanzania.
KUHUSU SCANIA TANZANIA LIMITED
Kampuni
ya Scania Tanzania inafanya kazi kama kampuni ndogo ya Scana CV AB yenye makao
makuu yake nchini Sweden. Kampuni ya Scania Tanzania inajihusisha na uingizaji
na usambazaji wa bidhaa za Scania nchini. Kampuni hii ina ofisi sehemu
mbalimbali nchini ambapo makao makuu yake ni Dar es Salaam, huku ofisi nyingine
ni Mwanza, Arusha na Mbeya.
Post a Comment