KAMATI YA SIASA WILAYA YA MOROGORO YAMPONGEZA DIWANI KATA YA MAZIMBU KWA UTEKELEZAJI BORA WA ILANI YA CCM.
Kiapo kikiendelea kufuatia mwanachama wa CHADEMA , Ndg. Peter Mgaya (kulia) kujiunga na CCM leo. |
Diwani wa Kata ya Mazimbu na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga akinyoosha juu Taarifa yake ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM akiwa na furaha huku wakisakata muziki. |
Diwani wa Kata ya Mazimbu, Mhe. Pascal Kihanga, akizungumza mbele ya Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini, Ndg. |
Fikiri
Juma (kulia) mara baada ya kutembelea ujenzi wa madaras aya Shule ya Sekondari
Kihonda.
Kamati ya Siasa Wilaya ya Morogoro Mjini ikiongozwa na Mwenyekiti Ndg. Fikiri Juma wakiwa katika Shule ya Msingi mazimbu A wakiongozwa na Diwani wa Kata hiyo, Mhe. Pascal Kihanga. |
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mazimbu A akitoa taarifa fupi ya Shule hiyo mbele ya Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini, Ndg. Fikiri Juma na Diwani wa Kata ya Mazimbu , Mhe. Pascal Kihanga. |
Zahanati ya Kata ya Mazimbu ikiwa katika haatua ya upauaji. |
Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini, Comrade Maulid Chambilila akizungumza kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini, Ndg. Fikiri Juma kuzungumza na Wana CCM. |
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini, Ndg. Fikiri Juma , akipokea Kadi ya aliyekuwa Mwanachama wa Chama Cha CHADEMA , Peter Mgaya, baada ya kujiunga na CCM leo. |
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya
Morogoro Mjini, Ndg. Fikiri Juma , akimkabidhi ya CCM aliyekuwa Mwanachama wa
Chama Cha CHADEMA , Peter Mgaya, baada ya kujiunga na CCM leo.
|
Kamati ya Siasa ya Wilaya ya
Morogoro Mjini, ikiongozwa na Mwenyekiti Fikiri Juma, imempongeza Diwani wa Kata ya Mazimbu ambaye ni Mstahiki Meya
wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga,pamoja na uongozi
wa Kata hiyo kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo na
utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi.
Mwenyekiti wa Kamati ya
Siasa Wilaya ya Morogoro Mjini, Ndg. Fikiri Juma, ametoa pongezi hizo leo Machi
14, 2020 kwenye Mkutano wa Diwani
aliouandaa kwa ajili ya kusoma taarifa za Utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM) katika kipindi chake cha muda wa miaka 4 tangia aingie madarakani
chini ya Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano, ya Mhe. Dkt. John Pombe
Magufuli.
Akizungumza na Wanachama
waliojitokeza katika mkutano huo ulioandaliwa na Diwani wa Kata ya Mazimbu,
Fikiri amesema kuwa amefurahishwa na
ubora wa miradi waliyoikagua katika Kata hiyo.
“ Tumefurahi kuona
Viongozi na wataalamu wanatusaidia kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi
ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2015/2020 kuhakikisha kile tulichoahidi wananchi
kimetekelezwa kwa asilimia kubwa na hivyo kuturahisishia majibu kwa wananchi,
lakini ningependa kuwaomba Viongozi wa Chama na Serikali zidisheni upendo na
ushirikiano bora wenye tija katika kutatua kero za wananchi wenu waliwaamini
wakiamini kuwa mnaweza sasa fanyeni kazi msitegeane maendeleo hayana chama ” Amesema
Fikiri.
“Niwapongeza sana Kamati
ya Maendeleo ya Kata kwa kushirikiana na
Chama pamoja na Serikali kuibua miradi mikubwa kama hii kwa ajili ya maendeleo
ya wananchi wenu, kwani Serikali imewekeza fedha nyingi pamoja na nguvu ya
wananchi , kwahiyo niseme mmefanya vitu vyenye uhakika sisi kama Wilaya tumeridhika na hiki tulichokiona, umoja wenu
unadhiilisha kuwa mpo vizuri, asanteni wote kwa kazi nzuri.” Ameongeza Fikiri.
Amesema kuwa kitendo cha
kwenda kukagua miradi katika Kata hiyo kabla ya kuanza mkutano ni miongoni mwa
majukumu yao yenye lengo la kukagua miradi ya maendeleo kama ilivyoahidiwa na
chama cha mapinduzi (CCM) wakati wa kampeni za uchaguzi za mwaka 2015 kwa lengo
la kujua utekelezaji wa ilani ya chama.
Kwa
upande wa Diwani wa Kata ya Mazimbu na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro,
Mhe. Pascal Kihanga, ameishukuru kamati ya siasa kwa ushirikiano wao na kuahidi
kuendelea kusimamia kwa makini zaidi miradi hiyo katika kuunga mkono juhudi za
Mhe. Rais Dkt. John Magufuli.
Amesema
kuwa tangia aingie madarakani mwaka 2015, kuna miradi ilikuwa haijatekelezwa lakini kwa
jitihada zake yapo mambo mbalimbali ameyafanya nakuleta maendeleo katika Kata
hiyo.
Amesema
miradi ya maendeleo walioifanya na Uongozi wake wa Kata imeonyesha dhahiri kwamba
Ilani ya CCM imetekelezwa kwa mafanikio makubwa sana na kuthibitisha jinsi
ambavyo Serikali ya Awamu ya Tano Chini ya Uongozi wa Mhe. Dkt John Magufuli
inavyowaletea Wananchi Maendeleo ya uhakika kwenye Kata ya Mazimbu , Mkoa wa
Morogoro na Tanzania kwa ujumla.
Amesema
kuwa Kata ya Mazimbu ina Shule za Serikali tatu, ambapo kati ya hizo Shule
mbili ni za msingi yaani Mazimbu A na B pamoja na Shule ya Sekondari Kihonda .
Aidha
amesema miongoni mwa usimamizi wa Shule za Msingi Mazimbu A mambo
yaliyotekelezwa ni pamoja na kuhamasisha ujenzi wa Chumba cha Kompyuta
kilichojengwa mwaka 2017 na kukamilika 2019, kuhamasisha ujenzi wa Chumba cha
darasa kilichojenwa tangu Disemba 2018 na kukamilika 2019 Julai ambapo wananchi
walichangia Shilingi 8,000,000/= na Serikali ilitoa Shilingi Milioni
12,500,000/=, amechangia uwekeaji wa umeme shuleni hapo kwa kutoa shilingi
495,000/=, kutafuta wafadhili wa kujenga na kununua tanki la maji lenye ujazo
wa lIta 2000 kwa Shule Mazimbu A amewezesha kufanya mitihani kwa darasa la saba
kwa kutoa shilingi 100,000/=, alitoa motisha kwa Waalimu baada ya ufaulu mzuri
kwa matokeo ya darasa la sabaya mwaka 2017 na 2018 kwa kutoa shilingi laki 5,000,000/=pamoja na
kutoa madawati 10 yenye thamani ya shilingi 1,000.000/=.
Amesema
kwa kutambua na kuthamini i kazi kubwa zinazofanywa na Ofisi ya Afisa Mtendaji
amehamasisha na kusimamia ukarabati wa Ofisi hiyo ya Kata ambayo pamoja na
ukongwe wa Ofisi hiyo pia ilikuwa inavuja sana hali iliyokuwa ikipelekea kulowa
kwa nyaraka mbalimbali na uharibifu mwengine mwingi ambapo kwa sasa Ofisi hiyo
iko vizuri licha ya kuhitaji ukamilishwaji.
Kwa
upande wa Shule ya Msingi Mazimbu B, miongoni mwa vitu alivyovitekeleza ni
pamoja na kuhamasisha kuongeza chumba kimoja cha darasa ambacho kimekamilika na
tayari wanafunzi wameanza kukitumia, kuhamasisha uwekaji wa umeme kwenye Ofisi
ya Mwalimu Mkuu pamoja na Ofisi ya Waalimu, kutafuta wafadhili wa kujenga na
kununua tanki la maji lenye ujazo wa lIta 2000, kuhamasiha na kusimamia
ukarabati wa matundu ya vyoo, kuhamasiha ukarabati wa vyumba vya madara kwa
kupiga rangi madarasa yote, kuhamasisha uanzishwaji wa madarasa ya vyumba
viwili ambavyo vimefikia hatua ya madirisha ambapo chini ya usimamizi wake pia
ufaulu wawanafunzi wa darasa la saba kwenda kidato cha kwanza umeongezeka kutoka
asilimia 97.47% hadi kufikia asilimia 100%.
Kuhusu
Sekta ya Afya, Chini ya Uongozi wa Mhe. Pascal Kihanga Kata ya Mazimbu haikuwa na Zahanati
lakini kwa sasa tayari wameshaanza ujenzi na Mhe. Kihanga amechangia kiasi cha Shilingi laki tatu (300,000/=)
katika kuunga mkono ujenzi wa Zahanati ya Kata ya Mazimbu ambapo ujenzi huo unaoendelea na kwa sasa umefikia hatua ya upauaji
Kwa
upande wa Sekta ya Mazingira , Mhe.Kihanga, amehamasisha uasfi wa mazingira
kwenye Mitaa yote na kwa kusimamia kanuni na miongozo mbalimbali ya Halmashauri
kwa kushirikiana na Baraza la Maendeleo la Kata wamehakikisha kuwa kinapatikana
Kikundi kimoja cha Usafi Msimamo Group huku akiendelea kushirikiana na Viongozi
wa ngazi zote kuhakikisha kuwa usafi wa mazingira unaboreka katika Kata ya
Mazimbu.
Aidha,
Mhe. Kihanga hakuacha mbali Sekta ya Miundombinu ambapo ametekeleza mabo kama
vile marekebisho ya mara kwa mara ya barabara itokayo Mataa hadi Ipoipo,
uwekaji wa kivuko cha wapiti kwa miguu Barabara ya FK, Ujenzi wa barabara ya
Barakuda kwa kiwango cha Lami, ambapo kwa kutambua adha wanazozipata wananchi
wake na kuwajali alihamasisha na kuchangia ufukuaji wa Mto Ngerengere ambapo
mto huo ulifukuliwa ili kuongeza kina na kuupa muelekeo mto huo kuzuia
uzaagaaji wa maji na kuingia kwenye makazi ya wananchi.
Kwa
upande wa Ulinzi na Usalama, Mhe. Kihanga ,ameendelea kushirikiana na Uongozi
wa Serikali za Miataa na Kata kuhakikisha kuwa ulinzi unaimarishwa katika
maeneo yote ambapo kwa kushirikiana na Mtendaji wa Kata na Baraza la Maendeleo
la Kata wamehakikisha Kata imepata Polisi Kata ambaye amekuwa akitoa
ushirikiano mkubwa kuhakikisha ulinzi na usalama unaimarika.
Kuhusua
Sekta ya Maendeleo ya Jamii, Mhe. Kihanga,amehamasisha Vijana , Wanawake na
watu wenye ulemavu kujiunga na kwenye vikundi na kusimamia na kuhakikisha wanapatiwa
mikopo ya Halmashauri , ambapo mwaka 2016 Vikundi vya Neema Group (Modeco a, Youth and Woman Association
(Modeco B), UWT Vicoba (Mazimbu darajani), na Agro Interprises (Mazimbu
darajani), mwaka 2017 UWT (Boma B), Mazimbu Vijana Spider (Boma A), WEMAMA
Group (Boma A) na watengeneza majiko (Modeco A), Mwaka 2018 Tushikamane
Wanawake (Nguzo), Morogoro Carvings, Mazimbu Vijana Spider (Boma A) na Mazimbu
Darajani Vicoba na Youth Organization (Reli), Mwaka 2019 Wanawake wapambanaji
(Boma A), Tumaini Group (Modeco B) na Nyota njema (Modeco A) huku akivipongeza vikundi vya Wanawake kwa
kuwa mastari wa mbele kurejesha fedha .
Lakini
Mhe. Kihanga hakuwa nyuma sana kwani amekuwa mstari wa mbele kuunga mkono
juhudi mbalimbali za kimaendeleo ndani ya Kata , huku kila mwaka akichangia Siku
ya Maadhimisho ya Wanawake Duniani ambayo Kata ya Mazimbu huadhimisha kabla ya
kilele cha jumla ambapo mwaka 2017/2018 alitoa shilingi 50,000/=, Mwaka 2019 alijitolea
utengenezaji wa madawati ambayo wakina mama walikabidhi katika Shule ya Msingi
Mazimbu A pamoja na pesa Shilingi 50,000/= huku mwaka huu akichangia shilingi
50,000/= wakina mama walipotembelea Walemavu wa Kituo cha Mehayo pamoja na
kuhudhuria maadhimisho hayo.
Mhe.
Kihanga kwa kutambua umuhimu wa michezo ameendesha Ligi ya Vijana ambayo
ilihusisha timu kutoka Mitaa yote saba ndani ya Kata ya Mazimbu ambapo
alijitolea Jezi kwa timu zote saba na mpira mmoja kwa kila timu huku akitoa
misaada mbalimbali ya kimichezo ikiwa ni pamoja na kuwafadhili mipira miwili
Shule ya Msingi Mazimbu A na B.
Aidha,
amesema kuwa kipimo cha Uongozi ni pale mtu anapopewa maelekezo akayafanyie
kazi na kama hajayafanyia kazi basi mtu huyo hatoshi kuitwa Kiongozi.
Amewataka
Wenyeviti wapya wa Serikali za Mitaa waige mazuri waliyokuwa wakiyafanya
waliowatangulia kwani mambo asilimia kubwa ya maendeleo yaliyopatikana katika
Kata hiyo yametokana na jitihada zao katika kushirikiana
Hata
hivyo amechukua nafasi ya kumpongeza Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. John Magufuli, kwa kuipatia Manispaa ya Morogoro fedha za miradi
ya Maendeleo hususani miradi ya Kimkakati.
Miongoni
mwa miradi aliyoitaja iliyotekelezwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro
ni pamoja na Ujenzi wa Soko Kuu la Kisasa, Stendi ya Msamvu, Stendi mpya ya
Daladala Mafiga, Stendi ya daladala Kaloleni, Jengo la Kitega uchumi DDC, Mto
Kikundi
Katika
ziara ya kamati ya Siasa ya Wilaya ya Morogoro Mjini miradi iliyotembelewa ni
pamoja na miradi ya Afya, Elimu, na Miundombinu,
Naye
Mwenyekiti wa CCM Kata ya Mazimbu, Liberati Njaru, amesema kuwa , Diwani
Kihanga, amekuwa akishirikiana na jamii nzima pasipo kujali itikadi za kisiasa
, dini wala jinsia katika shughuli mbalimbali za shida na raha zinapotokea
pamoja na kuwasaidia wanaopatwa na majanga mbalimbali na misiba
“Tumepata
Diwani CCM tunaomba mturudidhie huyu mtu kwani amekuwa karibu sana na
mtekelezaji mkubwa wa shughuli za Chama Cha Mapinduzi kuanzia ngazi ya Shina
hadi Kata , amekuwa akishiriki kwa hali na mali katika kuhudhuria na kuchangia
katika shughuli mbalimbali za Chama na Jumuiya zake” Amesema Njaru.
Post a Comment