DC CHONJO ASAMBAZA NDOO 100 ZA KUNAWIA MAJI MANISPAA YA MOROGORO KATIKA KUJIKINGA NA UGONJWA WA CORONA.
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Regina Chonjo, akizungumza na Wananchi wa Stendi ya Daladala Mjini wakati wa zoezi la kuwakabidhi Ndoo pamoja na sabuni zilizodhaminiwa na Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini, Mhe. Abdulaziz Abood kwa ajili ya kujikinga na Ugonjwa wa CORONA.
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Regina Chonjo, akimkabidhi ndoo mmoja wa viongozi wa Bodaboda Stendi ya Daladala Mjini , (katikati) ni Katibu wa Mbunge Jimbo la Morogoro Mjini, Ndg. Moses. |
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, mhe. Regina Chonjo, akizungumza na Wauza Matunda katika Kijiwe cha Stendi ya Bajaji (JUMATA) katika kutoa elimu juu ya kujikinga na Ugonjwa wa CORONA. |
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Regina Chonjo, akimkabidhi ndoo mmoja wa Viongozi wa Soko la Manzese. |
Mtaalamu wa afya Manispaa ya Morogoro, akiendelea kutoa elimu kwa Wananchi Juu ya kujikinga na Ugonjwa wa CORONA. |
MKUU wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Regina Chonjo,amekabidhi
jumla ya Ndoo 100 za kuwekea maji tirirka pamoja na sabuni katika kujikinga na
Ugonjwa wa CORONA Manispaa ya Morogoro.
Akizungumza na Waandishi wa habari, amesema kuwa ndoo hizo
zimenunuliwa chini ya ufadhili wa Mbunge wa Jimbo Morogoro Mjini,Mhe. Abdulaziz
Abood katika kuhakikisha Wananchi wa Jimbo lake wanajikinga na Ugonjwa wa
CORONA.
Amesema kuwa ni jukumu la Wananchi kuzitunza ndoo hizo ili
ziendelee kutumika katika maeneo yao ya biashara.
Aidha, amesema Ndoo hizo sio mali ya mtu binafsi bali kila
mtu atakuwa na haki ya kuitumia ili kuweza kusaidia katika kujikinga na
Maambukizi ya Virusi vya CORONA COVIC -19.
“Leo tunagawa Ndoo hizi katika maeneo tofauti tofauti,
kikubwa niwaombe Wananchi kwamba wawe wastaarabu katika kuvitunza isitokee mtu
akakichukua akajifanya ni ya kwake, Mhe. Wenu Abood anawapenda sana , katika
kuona janga hili linakuwa halina madhara ameona ni vyema akaungana na Wananchi
wake kuwasidia ili katotumia ile pesa ambayo ni mitaji yenu msiitumie badala yake
ametoa ndoo hizi na sabuni, kikubwa elimu iendelee kutolewa na sisi wenyewe
tuwe mabalozi wazuri wa kuelimishana juu ya kujikinga na Ugonjwa huu ambao ni
hatari sana ukiangalia Mataifa ya wenzetu wanateketea sana hivyo lazima na sisi
tuchukue tahadhari kubwa ya kujikinga ili tuwe salama”Amesema DC Chonjo.
Kwa upande wa Mwananchi, Juma Abdallah, amempongeza Mkuu wa
Wilaya ya Morogoro pamoja na Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini, Mhe. Abdulaziz
Abood kwa kuwapatia ndoo na sabuni.
“Tunawashukuru sana Viongozi wetu kwa kuonesha moyo wa
kutujali sisi katika vijiwe vyetu tumekuwa tukipeana sana elimu lakini ujio wako
tena kwa kutupatia vifaa kama hivi umetufariji sana, sasa tunaungana na Serikali
yetu kupaza sauti kwa pamoja ili kuhakikisha kila mwananchi anajikinga na
ugonjwa huu na kufanya Taifa letu kuwa
salama hususani katika Manispaa yetu ya
Morogoro” Amesema Juma.
Pia amechukua nafasi ya Kupongeza Jitihada zinazofanywa na
Uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro chini ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Sheila Lukuba pamoja na Mganga Mkuu wa Manispaa ya Morogoro , Dr Ikaji Rashid na timu nzima ya Wataalamu wa Afya kuanzia Ngazi ya Wilaya, Manispaa na Kata hadi kwenye Mitaa kwa jitihada kubwa za kutoa elimu dhidi ya
kujikinga na Ugonjwa wa CORONA.
Miongoni mwa maeneo ambayo ndoo hizo zilisambazwa ni pamoja na Stendi ya Daladala Mjini, Stendi ya Bajaji (Jumata) na Wauza Matunda, Soko la Manzese na Vijiwe vya Bodaboda, Soko la Fire Kiwanja cha Ndege, Masika, Stendi ya Daladala Kaloleni, Stendi ya Mabasi Msamvu na maegesho ya Magari ya kukodishwa nje ya Stendi ya Msamvu, Kihonda viwandani, Mazimbu Road, Kihonda kwa Chambo, Barabara ya Ipo Ipo, Soko la Mazimbu jirani na Ofisi ya Kata ya Mazimbu, Chamwino pamoja na Soko la Chamwino.
Miongoni mwa maeneo ambayo ndoo hizo zilisambazwa ni pamoja na Stendi ya Daladala Mjini, Stendi ya Bajaji (Jumata) na Wauza Matunda, Soko la Manzese na Vijiwe vya Bodaboda, Soko la Fire Kiwanja cha Ndege, Masika, Stendi ya Daladala Kaloleni, Stendi ya Mabasi Msamvu na maegesho ya Magari ya kukodishwa nje ya Stendi ya Msamvu, Kihonda viwandani, Mazimbu Road, Kihonda kwa Chambo, Barabara ya Ipo Ipo, Soko la Mazimbu jirani na Ofisi ya Kata ya Mazimbu, Chamwino pamoja na Soko la Chamwino.
Post a Comment