AFISA UTUMISHI MANISPAA YA MOROGORO AKUTANA NA MAAFISA AFYA NA WATENDAJI KATA KUFANYA TATHIMINI NA HATUA ZILIZOCHUKULIWA KATIKA KATA DHIDI YA KUJIKINGA NA UGONJWA WA CORONA COVIC-19 .
Afisa Afya Manispaa ya Morogoro, Prisca Gallet, akizungumza na Watendaji pamoja na Maafisa Afya. |
Afisa Afya Manispaa ya Morogoro, Prisca Gallet, akitoa elimu ya Ugonjwa CORONA COVIC-19 kwa Watendaji pamoja na Maafisa Afya. |
Mmoja wa Watendaji wa Kata akichangia hoja ya nini kifanyike katika kuelimisha zaidi wananchi dhid ya maambukizi ya Virusi vya CORONA. |
AFISA Utumishi Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, Waziri
Kombo , amekutana na Watendaji wa Kata zote 29 pamoja na Watendaji wa Mitaa,
Maafisa Afya kwa ajili ya kuwasilisha taarifa za jinsi gani walivyochukua hatua
katika maeneo yao dhidi ya kujikinga na Ugonjwa wa CORONA.
Mkutano huo wa kuwasilisha taarifa na kujadiliana juu ya
kujikinga na Ugonjwa wa CORONA umefanyikika leo Machi 26 , 2020 katika Ukumbi
wa Mikutano wa Manispaa ya Morogoro.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro,
amesema lengo la mkutano huo ni kufanya tathimini juu ya hatua zilizochukuliwa
na Maafisa Afya wa Kata pamoja na Watendaji dhidi ya
kujikinga na Ugonjwa wa CORONA.
Amesema tangia Serikali itangaze taratibu za Kujikinga , kwa
upande wa Manispaa hali ya utoaji wa elimu imefanyika kwa kiasi kikubwa sana
na mapokeo ni mazuri licha ya kuwepo kwa maeneo machache ambayo yamekuwa chini
sana katika mapokeo ya kujikinga dhidi ya ugonjwa huo.
Aidha, amewataka Maafisa Afya pamoja na Watendaji
kushirikiana kikamilifu na kuunda timu ndogo ambayo ikatakuwa inafanya
ufuatiliaji kuanzia ngazi zote na maeneeo yote ambayo yana mkusanyiko, kwenye
maduka, Hoteli, Nyumba za Ibada pamoja na Stendi za Mabasi ili kuoana hali ya
utekelezaji ikoje katika maeneo hayo.
“Kiujumla katika Manispaa yetu ya Morogoro tumejitahidi sana
kuelimisha Wananchi , tumekuwa tukitumia njia mbalimbali kama vile matangazo
ya vipeperushe, Magari mitaani, Vyombo vya habari, lakini sasa tumekwenda mbali zaidi kwa kugawana majukumu na kuunda timu tatu ambazo zitakuwa zikifanya kazi
za ufuatiliaji ikiwemo timu itakayopitia Hotelini, Vitu vya Mabasi na Bodaboda
na ile itakayopitia katika Maduka ya Dawa na kawaida ili kuona kama Vitakasa
mikono vinazingatia bei elekezi ya Serikali” Amesema Kombo.
Hata hivyo ametoa agizo kwa Maafisa Afya wote na Watendaji
katika ngazi za Kata na Mitaa kuhakikisha kila mwezi wanatoa taarifa jinsi gani
wameshughulikia suala hilo kikamilifu katika maeneo yao na taarifa hizo
ziwasilishwe kwa Afisa Afya wa Manispaa ambaye atatoa fomu maalumu za kujaza.
Naye Afisa Afya Manispaa ya Morogoro, Prisca Gallet, ameipongeza
timu ya Waatalamu pamoja na Maafisa Afya wa Kata na Watendaji kwa jitihada
walizochukua za kutoa elimu ya kujikinga na Ugonjwa wa CORONA licha ya kuwepo
na changamoto za baadhi ya maeneo kutofuata taratibu hizo.
Amesema mipango iliyopo ni kuhakikisha maeneo yote yaliyopo
Manispaa ya Morogoro yanatenga Maji tiririkia na sabuni pamoja na Vitakasa
Mikono na kwa wale watakao kaidi watachukuliwa hatua kali za kisheria.
‘Tumeanza kuona matokeo mazuri, hata katika pita pita yangu
nimeona tunajitahidi hongereni sana wataalamu , lakini tusibweteke Ugonjwa huu
kama mnavyojua ni mgeni katika Nchi yetu , sasa tuanakila sababu za kufuata maelekezo ya Viongozi
wetu wa Ngazi za Juu pamoja na Wataalamu wetu wa Afya, tukifanya hivyo na kila
mtu akifanya kwa nafasi yake tutakuwa salama katika kujikinga na Ugonjwa huu,
kikubwa Maafisa Afya na Watendaji mshirikiane kikamilifu na kila Kata ichukue
tahadhari kubwa ya kuwaelimisha Wananchi wake”Amesema Gallet.
Post a Comment