Header Ads

Maadhimisho ya siku ya furaha Duniani, Mkurugenzi Manispaa ya Morogoro atoa neno kwa watumishi.



Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba, amewataka  watumishi kudumisha upendo kazini katika kuleta maendeleo.

Hayo ameyazungumza leo Machi 19, 2020 ikiwa ni siku moja klaba ya kuadhimisha Siku ya Furaha Duniani ambayo kila ifikapo Machi 20 ya kila mwaka maadhimisho hayo hufanyika duniani kote.

Sheilla, amesema kama upendo na amani pamoja na furaha vikudumishwa Ofisini basi maendeleo ni rahisi kuja kutokana na ushirikiano utaoonyeshwa na Wafanyakazi ambapo amesema mara nyingi kukosekana na kwa furaha ni miongoni mwa njia ya  kukosa nguvu ya pamoja na kuchangia kushuka kwa maendeleo na malengo mahususi yaliyopangwa.

Amesema kuwa, kutafuta furaha ni moja ya lengo kuu msingi wa maisha ya binadamu na zaidi ni kutambua mbinu inayojumuisha zaidi ya usawa katika ukuaji wa uchumi na ambao kwa dhati unalenga maendeleo endelevu ya mwanadamu.

"Katika maadhimisho haya, nipende kuwaomba watumishi hususani katika Manispaa ya Morogoro, tujenge utamaduni wa kupendana wenye kwa wenyewe, tukipenda tutaimarisha mahusiano bora zaidi katika nyanja za maendeleo na hatimaye kuwe

ka nguvu ya pamoja ya kusongesha Manispaa yetu mbele kimaendeleo na kufikia malengo tuliyojiwekea, lakini kama furaha itakosekana ndani yetu hata ushirikiano wa pamoja tutaukosa na tutachelewa kufikia malengo, kikubwa tufanye kazi kwa bidii, tutii sheria, kanuni na miongozi kazini na tusimamie malengo yetu  bila kuyumbishwa ili wananchi wa Manispaa yetu waone matunda na kumsaidia Mhe. Rais . Dkt. John Pombe Magufuli. katika adhima ya Tanzania ya Viwanda na Uchumi wa Kati" Amesema Sheilla.

Amesema furaha ikiwepo hata ile hali ya kujikuta wewe ni masikini na unashindwa kufikia malengo inatoweka na  hatimaye hali hiyo ya furaha inamfanya mtu aweze kuwa sawa na watu wote na hali hiyo pia ni  zaidi ni moja ya mambo mengine ya kumwezesha mwanadamu aonje kweli ustawi wa  maisha yake katika jamii.

Amesema Umoja wa Mataifa na mashirika mengine ya kimataifa na kikanda, pamoja na mashirika ya kiraia, yakiwemo yale mashirika yasiyo ya kiserikali na watu binafsi,waliamua  kusherehekea sikukuu ya Siku ya Furaha duniani kwa namna inayofaa, hata kwa njia ya kufanya shughuli  za pamoja zinazolenga elimu, ili kukuza ufahamu katika umma.

Pia amesema kwa asili, suala la kutafuta furaha linawakilisha moja ya haki za msingi kabisa za kibinadamu na lengo msingi la maisha ya binadamu!


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.