RAS MOROGORO AWATAKA WAJASIRIAMALI WANAWAKE KUIBUA MIRADI YENYE TIJA NA KUTEKELEZEKA ILI KUREJESHA MIKOPO KWA WAKATI.
Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro, Mhandisi Emmanuel Kalobelo, akimkabidhi cheti cha pongezi mmoja wa wadau walifanikisha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyoandaliwa na Manispaa ya Morogoro. |
KATIBU Tawala Mkoa wa Morogoro, Mhandisi Eng. Emmanuel
Kalobelo, amewataka Wakina Mama Wajasiriamali kuibua miradi yenye tija na inayotekelezeka
ili kuweza kurejesha fedha za mikopo kwa wakati kuliko kuwa na biashara ambazo
haziwezi kuwapatia faida kwa wakati.
Ameyasema hayo wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake
Duniani yaliyoandaliwa na Halmashauri ya
Manispaa ya Morogoro yaliyofanyika katika Uwanja wa Mpira wa Jamhuri
Machi 8, 2020.
Akizungumza na Wakina Mama na Wanawake waliojitokeza katika
Maadhimisho hayo, amesema Wajasiriamali wanapaswa kubadilika na kubuni biashara
kubwa ambapo watakopeshwa vifaaa badala ya fedha kwani Serikali ipo tayari
kuwawezesha kununua Vifaa na Mashine za kuendeshea shughuli zao za uzalishaji.
Amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya
Uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli , imepitisha Sheria ya utoaji wa
mikopo kwa Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu na kutengeneza kanuni za uendeshaji wa mfuko wa mkopo, ambapo
sheria hiyo imeelekeza kila Halmashauri kutenga asilimia 10 ya mapato yake ya
ndani ili kutoa mikopo isiyo na riba kwa makundi ya wanawake asilimia 4,,
Vijana asilimia 4 na Watu wenye Ulemavu asilimia 2.
Pia amesema zoezi la utoaji wav yeti vya pongezi
lililofanywa na Manispaa ya Morogoro litakuwa endelevu kwa kutoa vyeti na tuzo
mbalimbali kwa Vikundi vinavyofanya vizuri.
Amesema Vikundi vya Wajasiriamali vinatambua nia ya Serikali
ya kukopesha Wajasiriamali wadogo ambao wanakosa fursa za kupata mikopo katika
taasisi mbalimbali za kifedha ikiwemo Benki.
“Wakina pamoja na
Wajasiriamali nawapongeza wote kwa
juhudi za uzalishaji mali na mshikamano mnaouonesha katika kujenga Halmashauri
yenu hususani katika suala zima la maendeleo, hii imepelekea Halmashauri yenu kusonga mbele katika
utekelezaji wa miradi ya Maendeleo ambayo inavutia na kuweza hata Halmashauri
nyingine kuja kujifunza kwenu hongereni sana, nimetoa hundi yenye thamani ya
Shilingi Milioni 100,000,000 mnatakiwa fedha hizi kuzitumia kwa lengo mjitahidi
kuwa waaminifu na kurejesha kwa wakati ili kutoa fursa kwa vikundi vyengine ”.
Amesema Kalobelo.
“Kuna vikundi ambavyo vimefanya vizuri sana na vimerejesha
mikopo kwa wakati na wanastahili pongezi, name nichukue fursa hii kwa kufanya kazi kwa bidii na kuzalisha
lakini pia mmeonesha uaminifu katika matumizi ya fedha hizi za mkopo, ni
dhahiri mmeweza kuongeza na kukuza mitaji yenu
hata mkaweza kurejesha kwa wakati, wengine wote ambao bado mnadaiwa
mjitahidi kurejesha kwa wakati ili kutoa fursa kwa wengine waweze kunufaika na
mkopo huu, ni kuombe Mkurugenzi wa
Manispaa uendelee kutenga asilimia 10 ya mapato ya ndani ili muwakopeshe wajasiriamali
hawa wanaotafuta mitaji ya kukuza biashara zao ” Ameongeza Kalobelo.
Amesema kuwa ili kuleta mapinduzi yaliyo ya kweli nay a Kimaendeleo
lazima uwekezaji ufanyike kwenye shughuli zinazoendana na na uanzishwaji wa
Viwanda, kama sera ya nchi inavyoelekeza aliyoionyesha Mhe. Rais Dkt John
Magufuli ya kauli mbiu ya hapa kazi tuu na kumuunga mkono kwa kutekeleza kwa
vitendo ambapo katika awamu hii wanawake
wamepewa nafasi kubwa kama nguvu kazi , wazalishaji na walezi wakubwa katika
familia na kuwaomba wasimuangushe Mhe. Rais wafanye kazi kwa bidii na kuweka
mikakati mizuri ya uzalishaji mali kwa kushirikiana na wanaume zao kuanzia
ngazi ya familia na kusongesha Taiafa mbele kiuchumi.
Aidha , amewataka Wanawake waangalie maendeleo ya familia
zao kwa ujumla katika Nyanja zote kwani usawa au kutokuwa na usawa chimbuko
lake linaanzia katika ngazi ya familia ambapo mfumo dume unazaliwa na
kuendelezwa.
Amesema ni muhimu wanawake wakashirikiana kwa pamoja na
wanaume zao katika suala zima la malezi katika familia zao ili kujenga kizazi
kinachozingatia usawa kuanzia watoto wakiwa wadogo hadi watakapokuwa watu
wazima na hii itasaidia kufikia malengo
ya maendeleo endelevu wanayoyatarajia.
Pia amechukua fursa ya kuwakumbusha wakina mama waendelee
kukemea vitendo vay ukatilia wa kijinsia vinavyoendelea katika jamii.
Pia amesisitiza ushirikiano wa kamati za kupinga na
kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto katika ngazi za mitaa,
Kata hadi Manispaa kushirikiana na Jeshi la Polisi Dawati la Jinsia katika
kutoa elimu ya masuala ya ukatili na kutoa taarifa za matukio ya ukatili
yanayofanyika katika maeneo yakiwemo ubakaji na ulawiti ili hatua za kisheria
zichukuliwe kwa wanaotenda makosa hayo.
Amesema ukatili wa jinsia una madhara makubwa kwani
unasababisha ulemavu wa kudumu, maambukizi ya Virusi vay UKIMWI athari ya
kisaikolojia kwa watoto na hatimaye kurudisha nyuma maendeleo kwa mhanga wa
ukatili.
Ametoa wito kwa wanawake na kuwaeleza kuwa Serikali chini ya
Rais Dkt. John Magufuli, imeanzisha programu mbalimbali ikiwamo programu ya
Elimu bure, Bima ya Afya iliyoboreshwa (CHF), na mkakati wa utoaji wa yeti vya kuzaliwa kwa watoto wenye umri chini
ya miaka mitano na kuagiza idara zote zinazohusika na programu hizo kuhakikisha
wanasismamia huduma hizo ipasavyo na
kuwaasa wanawake kupitia mikutano yao ya
vikundi vya kijamii kama vile VICOBA, SACCOS wapeane taarifa za kimaendeleo na
wawe tayari kuhudhuria mikutano ya Mitaa
inayoandaliwa kwa mujibu wa sheria kwani huko ndiko chimbuko la taarifa za
imaendleeo na fursa mbalimbali zinazojitokeza.
Pia amewataka wataalamu na Viongozi wa Manispaa kuhakikisha
wanawatumia wenyeviti wa Mitaa vizuri na ikiwezekana uhamasishaji ufanyike
nyumba kwa nyumba ili wananchi wajiunge na CHF , Watoto chini ya miaka mitano
waandikishwe na kupatiwa vyeti vya kuzaliwa.
Hata hivyo amewataka wakina mama wajitokeze kwa wingi katika
kipindi cha uchaguzi mkuu Oktoba 2020 ili waweze kugombea nafasi za Uongozi
katika maeneo yao jambo amabalo litadhihirisha kwamba wanatekeleza kwa vitendo
kauli mbiu ya “KIZAZI CHA USAWA KWA MAENDELEO YA TANZANIA YA SASA NA YA BAADAYE”
huku akiwapongeza wanawake wote waliojitokeza katika kugombea nafasi uchaguzi
wa Serikali za Mitaa na waliojitokeza katika kujiandikisha kwenye daftari la
kudumu la wapiga kura.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa manispaa ya Morogoro, Sheilla
Lukuba, amesema Manispaa ya Morogoro inatambua na kuthamini juhudi zinazofanywa
na wajasiriamali wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu ambapo katika kipindi
cha fedha mwaka 2019/2020 manispaa imetoa kiasi cha shilingi milioni 100 kwa ajili
ya mikopo ambapo kati ya hizo shilingi milioni 45,5000,000.00/= zimetolewa kwa
vikundi 9 vya Wanawake, shilingi milioni 45,500,000.00/= kwa vikundi 11 vya
Vijana na shilingi milioni 9,000,000.00/= kwa vikundi 3 vya watu wenye ulemavu.
Ameishukuru Serikali kwa kuwapatia mikopo hiyo katika
kusukuma gurudumu mbele la maendeleo ya wananchi wa Manispaa ya Morogoro huku
akiwataka wanawake na wakina mama pamoja na vijana wale waliokuwa majumbqani
wajiunge vikundi ili waweze kupatiwa mikopo na kujimwamu kiuchumi.
Naye Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Morogoro, amesema
katika mwaka wa fedha wa 2018/2019 , Halmashauri ya Mnaispaa Morogoro ilitoa
mkopo wa Shilingi Milioni 402,500,000/= kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na
Watu wenye ulemavu ambapo vikundi 76 vya wanawake vilipatiwa mkopo wa shilingi
milioni 214,500,000/=, vikundi 51 vijana walipewa shilingi milioni
151,500,000/= na vikundi 13 vya watu wenye ulemavu walipewa shilingi milioni
36,500,000/=.
Amesema mpaka kufikia Oktoba 2019 vikundi 22 vya wanawake
vilipaswa viwe vimekamilisha marejesho , vikundi 12 pamoja na vikundi 11 vya
watu wenye ulemavu vyote vilipaswa viwe vinaelekea katika kurejesha fedha.
Amesema Manispaa ya Morogoro kupitia muunganiko wa wanawake
wajasiriamali vya jukwaa linaendesha darasa la ushonaji eneo la Tushikamane
ambapo hadi sasa jumla ya wanafunzi 20 wamemaliza awamu ya kwanza ya ushonaji
waliobaki ni wanafunzi 3 na kituo kinaelekea kusajili wanafunzi wengine.
Amesema kwa kipindi cha mwaka 2019/2020 kuanzia Julai hadi
kufikia mwezi Februali jumla ya vikundi 205 vimesajiliwa na kati aya hivyo
vikundi viwili vya Vijana vimeshapatiwa mkopo mna Manispaa.
Katika maadhimisho hayo miongoni mwa shughuli zilizokuwa
zikifanyika ni pamoja na Maonesho ya
bidahaa mbalimbali za wanawake zinazofanywa na wajasiriamali pamoja na shughuli
mbalimbali zinazofanywa na wadau , Elimu ya Jinsia na ukatili kwa wanafunzi wa
shule za Msingi na Sekondari, Huduma ya Msaada wa kisheria kwa wananchi wenye
uhitaji katika Kata ya Lukobe na Kata Jirani za Kihonda na Mkundi, Utoaji wa
msaada kwa kituo kimoja cha watoto yatima kituo cha Mgolole, kambi ya Wazee
Fungafunga, Gereza la wafungwa wanawake Kingolwira na kwa watoto wenye ulemavu wa akili kituo
cha Mehayo Kata ya Mazimbu, Upimaji wa Saratani ya shingo ya kizazi na VVU ,
Bonanza kwa Wananchi wa Mzinga na uchangiaji wa damu salama pamoja na
Mashindano ya michezo kwa wanawake ikiwemo kukimbiza kuku, kukimbia kwenye
gunia na kuvuta kamba.
Post a Comment