Header Ads

Uongozi wa Wamachinga Manispaa ya Morogoro waunga mkono jitihada za kujikinga na Ugonjwa wa CORONA.



Mwenyekiti wa Wamachinga Manispaa ya Morogoro, Faustine Almas, (aliyevaa tisheti ya kijivu) akiendelee kutoa elimu ya kunawa mikono kwa wafanyabiashara.


UONGOZI wa Wamachinga Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, imeunga mkono juhudi za kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Ugonjwa wa CORONA baada ya kuweka maji safi tiririka na sabuni katika Mitaa yote ya biashara zao .

Akizungumza na Waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Wamachinga Manispaa ya Morogoro, Faustine Almas , amesema kitendo cha kuweka maji tirirka na sabuni kila kona ya maenenso yao ya kibiashara ni kutokana na kutekekeleza na kuuunga mkono juhudi za Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Drkt. John Pombe Magufuli la kutaka maeneoe yote nchini yawe na maji tiririka na sabuni pamoja na vitakasa mikono kwa ajili ya kujikinga na Ugonjwa wa CORONA.

Aidha, ameupongeza Uongozi wa Manispaa ya Morogoro pamoja na timu nzima ya Wtaalamu wa Afya wa Manispaa  kwa jitihada za kutoa elimu dhidi ya kujikinga na Ugonjwa wa CORONA kwa kuzunguka maeneo yote ya Manispaa.

"Sisi Chama cha Wamachinga Manispaa ya Morogoro, tunapongeza sana juhudi za Viongozi wetu kuanzia ngazi za Kitaifa, Mkoa, Wilaya na Halmashauri kwa kazi kubwa ya kuelimisha jamii jinsi ya kujikinga na Ugonjwa wa CORONA , kwa maagizo ya Viongozi wa Juu nasi tukaona tutekeleze wajibu wetu wa kuweka ndoo za maji tiririka na sabuni pamoja na Sanitezer (vitakasa mikono) katika maeneo yote ya biashara zetu ili wateja wetu na wafanyabiashara waweze kunawa mikono na kujikinga na Ugonjwa huu, nampongze Mkuu wa Wilaya Mhe. Regina Chonjo amefanya kazi kubwa pamoja na Mkurugenzi wa Manispaa , Sheilla Lukuba, kwakweli Manispaa yetu elimu imeenea sana, niwaombe wenzetu ambao bado hawajachukua hatua hizi wafanye mara moja lakini  kikubwa tuzidi kujilinda na kumuomba Mwenyezi Mungu atuepushie mbali na ugonjwa huu" Amesema Faustine.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro,Sheilla Lukuba, ameupongeza Uongozi wa Wamachinga Manispaa ya Morogoro kwa jitihada walizozifanya za kuweka ndoo na maji tiririka kwa  kila kona ya maeneo yao ya biashara.

"Hili ni jambo jema sana, huku kwenye biashara ndio kuna mikusanyiko mingi ya watu, hivyo wamefanya jambo zuri la kuwalinda wafanyabisahara wao pamoja na wateja na timu yetu ya wataalamu wa afya bado ipo mitaani inazidi kutoa elimu, kikubwa niwaombe Wananchi wa Manispaa ya Morogoro, tusipuuze maagizo ya Wataalamu tuwe makini sana ile mikusanyiko tuache sasa na kama unasafiri uwe na safari ya kilazima kama huna kaa nyumbani tulia na maeneo mengine ya biashara muige wenzenu walivyofanya tukiwa wote tunafanya hivi tutajikinga na Ugonjwa huu na Manispaa yetu itakuwa salama" Amesema Sheilla.


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.