Header Ads

TANGAZO LA MWALIKO KWA WANANCHI WA MANISPAA YA MOROGORO SIKU YA WANAWAKE DUNIANI


Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba.
MKURUGENZI WA MANISPAA YA MOROGORO, SHEILLA LUKUBA, ANAWATANGAZIA WANANCHI WOTE WA MANISPAA YA MOROGORO KUHUDHURIA KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIA YATAKAYOFANYIKA KATIKA UWANJA WA MPIRA WA JAMHURI SIKU YA TAREHE 8/3/2020 AMBAPO MAADHIMISHO HAYO YATAAMBATANA NA MAANDAMANO YATAKAYOANZIA OFISI YA MANISPAA YA MOROGORO KUANZIA SAA 2:30 ASUBUHI .

MGENI RASMI KATIKA MAADHIMISHO HAYO ANATARAJIWA KUWA KATIBU TAWALA MKOA WA MOROGORO, MHANDISI EMMANUEL KALOBERO .

SHUGHULI ZITAKAZO FANYIKA KATIKA SIKU HIYO YA MAADHIMISHO NI PAMOJA NA MAONESHO YA BIDHAA ZINAZOZALISHWA NA WAJASIRIAMALI  NA SHUGHULI ZINAZOFANYWA NA WADAU, UPIMAJI WA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI NA VVU PAMOJA NA MICHEZO MBALIMBALI NA UTAMADUNI.

SAMBAMBA NA HAPO KUTAKUWA NA BURADI YA MUZIKI KUTOKA KWA WASANII WA SINGELI KAMA VILE SUNURA, MZEE WA BWAX PAMOJA NA MALIKIA WA MIPASHO NCHINI , HADIJA KOPA PAMOJA, VIKUNDI VYA NGOMA NA UTAMADUNI NA MCHUNGAJI MGOGO MTAALAMU WA MASUALA YA  KUELIMSHA WANAWAKE NA WAKINA MAMA JINSI YA KUJIKWAMUA KUCHUMI.

KAULI MBIU , "KIZAZI CHA USAWA KWA MAENDELEO YA TANZANIA YA SASA NA YA BAADAYE".

WOTE MNAKARIBISHWA.
Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Morogoro, Bi. Enedy Mwanakatwe.



No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.