Boda boda wapongeza juhudi zinazofanywa na Manispaa ya Morogoro juu ya utoaji wa elimu ya kujikinga na Ugonjwa wa CORONA.
Mmoja wa waendesha Boda boda akizungumza na kupongeza Manispaa ya Morogoro kwa jitihada wanazozifanya katika kuwapatia elimu ya kujikinga na Ugonjwa Corona. |
Mratibu wa Malaria na Magonjwa ya Watoto wenye umri chini ya miaka 5, Dr. Nicholaus Ntabaye (kushoto) akizungumza na Boda boda katika kituo cha Masika juu ya elimu ya kujikinga na Ugonjwa Corona. |
Afisa Ustawi wa Jamii wa Manispaa ya Morogoro, Sidina Mathias , akipuliza dawa kwenye kofia (elementi) ili kujikinga na Ugonjwa wa Corona. |
Katibu wa Boda boda Mkoa wa Morogoro, Juma Bega akiwa ameshikilia Boda boda iliyokuwa ikipuliziwa dawa . |
Afisa Lishe Manispaa ya Morogoro, Elina Kweka, akiwapulizia dawa ya vitakasa mikono waendesha Boda boda. |
WAENDESHA Boda boda
Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro wameipongeza Manispaa ya Morogoro kupitia
Idara ya Afya kwa jitihada za kuhamasisha na kutoa elimu juu ya kujikinga
na Ugonjwa wa CORONA.
Akizungumza kwa niaba ya Bodaboda wote, Katibu wa Bodaboda Mkoa wa Morogoro, Ndg. Juma Bega, amesema kitendo cha Manispaa kutenga muda wa kutembelea makundi maaalumu kama haya ya Vijana wao ni jambo jema na kuonyesha kwamba Serikali inawathamini Bodaboda na kuona kazi hiyo ni kama kazi nyengine zinazowaingizia vipato.
"Kwa kweli nichukue nafasi hii kwa niaba ya Uongozi wa Bodaboda Mkoa wa Morogoro, tunaipongeza sana Manispaa ya Morogoro hususani idara ya Afya chini ya ndugu yangu , Dr Ikaji Rashidi kwa kugawa maeneo ya kutolea elimu chini ya Wataalamu wake , hali hii imeonyesha upendo wa dhati na kuona sasa kundi hili linatambulika sana na kuweza kuokoa hata maisha ya Vijana wetu kwa kuwapatia Elimu hii ya kujikinga na Ugonjwa wa Corona, nampongeza sana Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mama yangu Regina Chonjo pamoja na Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro dada yangu Sheilla Lukuba kwa kuchukua hatua madhubuti kabisa na kuunga mkono kauli ya Mhe. Rais wetu Dkt. John Pombe Magufuli ya kutoa elimu na kuweka tahadahri kubwa katika nchi yetu ili kujikinga na Ugonjwa wa Corona" Amesema Bega.
Aidha , amewataka Bodaboda wote Mkoa wa Morogoro kuuchukilia Ugonjwa huo kwa umakini mkubwa na kuweka tahadhari za kujikinga wao na familia zao pamoja na abiria wanaowapakia kwa kunyunyiza dawa kwenye viti , mikono ya kushikia wakati wanaendesha pamoja na kupuliza dawa kwenye kofia zao na za abiria (elementi).
Kwa
upande wa Mratibu wa Malaria na Magonjwa ya Watoto wenye umri chini ya miaka 5,
Dr. Nicholaus Ntabaye akizungumza kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Manispaa ya
Morogoro, amesema kila Boda boda ni lazima ahakikishe chombo chake kabla ya
kukitumia anakipulizia dawa ikiwamo viti, sehemu za kushikia mikono pamoja na
kofia zao (elementi) ili kujikinga na Ugonjwa wa Corona.
"Nitoe wito kwa boda boda wote niwaombe msipuuzie haya maelekezo tumewafuata mlipo lengo letu ni kuwa karibu na wananchi wetu na kuangalia usalama wenu, zingatieni maelekezo ya wataalamu wanayowaambia huu ugonjwa sio mzuri hata kidogo wenzetu Mataifa ya nje wanateketea, tuwe makini sana na vyombo vyetu mara kwa mara tuviweke katika mazingira rafiki katika kujikinga na ugonjwa huu" Amesema Dr. Ntabaye.
Post a Comment