Manispaa ya Morogoro yawawakumbuka Watoto yatima Kituo cha Mgolole kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.
Viongozi wa Manispaa ya Morogoro wakiwa pamoja na Watoto wanaolelewa katika Makao ya Mgolole baada ya kutoa zawadi ya vyakula katika kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani. |
HALMASHAURI ya Manispaa ya Morogoro imefanya matembezi ya
kuwakumbuka Watoto Yatima na wanaoishi katika Mazingira kwa kutekeleza utoaji
wa zawadi wa Vyakula katika Makao ya kulelea watoto yatima na wanaoishi katika
mazingira magumu cha MGOLOLE kilichopo Manispaa ya Morogoro.
Akikabidhi vitu hivyo
vyenye thamani ya Shilingi laki 300000/= , kwa niaba ya Mkurugenzi, Afisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya
Morogoro, Sidna Mathias, amesema kuwa Manispaa ya Morogoro kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii kwa ujumla iko pamoja nao na itaendelea kushirikiana nao kwa mazuri na
changamoto yeyote katika makao hayo na wasisite kutoa taarifa pale
wanapokuwa na tatizo lolote.
Miongoni mwa vyakula vilivyotelewa ni pamoja na Samaki kilo 17 sawa na shilingi 135,000/=, Vitunguu maji kilo 20 sawa na shilingi 60,000/=, Vitunguu swaumu kilo 5 shilingi 40,000/=, Nyanya maji sado 5 shilingi 55,000/=.
“Nimmefurahishwa
sana na huduma mnazowapatia watoto wetu, kwakweli mnastahili pongezi kubwa ni
wachache wenye moyo kama wenu wa kuwasaidiahawa watoto, msikate tamaa
endeleeni na malezi bora mwenyezi mungu atawabariki sana chukueni hiki kidogo
tulichowaletea ikiwa ni sehemu yetu ya kusherekea maadhimisho ya Siku ya
Wanawake Duniani na watoto wetu
wajisikie huru na Amani badala ya kuwa wapweke”Amesema Sidna.
Kwa upande wa Mratibu wa Mratibu wa TASAF Manispaa ya Morogoro,
Feliciana Katemana , amesema kuwa huo ni mwendelezo wa
ushirikiano mzuri unaoendelea kufanyanywa na Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro ambapo Manispaa imekuwa
na utaratibu wa kuleta miasaada mbalimbali kwa kushirikina na Ofisi ya Mkuu wa
Wilaya na wadau wengine.
Amesema vyakula hivyo ni njia moja wapo ya kuwatia nguvu wale
wanaowalea Watoto na waendelee na moyo wa kuwasaidia watoto hao hadi
pale watakapo pata mwangaza wa maisha yao.
“Watoto niwaombe msome sana mkizingatia hakuna urithi Zaidi
ya elimu, Serikali ya awamu ya tano chini ya Mhe. Rais Dkt. John Magufuli
imewekka mpango wa elimu bila malipo msome sana ili nayi baadae muweze kuwa na
masiha mazuri na kuendesha familia zenu” Amesema Katemana.
Aidha, Katemana, amechukua nafasi kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, kuwakaribisha wananchi wa Manispaa ya Morogoro kujitokeza na kuhudhuria kwa wingi katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yatakayofanyika katika Uwanja wa Mpira wa Miguu wa Jamhuri siku ya Tarehe 8, Machi 2020 , Jumapili ambapo maadhimisho hayo yataambatana na Maandamano yatakayoanzia katika Ofisi ya Manispaa kuanzia saa 2:30 Asubuhi.
Naye, Mlezi wa Makao hayo, Sister Palagia Maria, ameushukuru
Uongozi wa Manispaa ya Morogoro ikiwamo Ustawi wa Jamii kwa kuwa karibu nao
huku akiwataka wasikate tamaa kwani wao wanategemea pia misaada kutoka kwa
wahisani.
Post a Comment