Waziri Jaffo aridhishwa na kazi za TARURA Manispaa ya Morogoro.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Selemani Jaffo, akikagua mfereji katika Barabara ya Arc Hotel. |
Waziri Jaffo akizungumza na kutoa maelekezo katika mradi wa Ujenzi wa Soko Kuu la Kisasa . |
Waziri Jaffo (kushoto) akiteta jambo na Afisa Utumishi wa Manispaa ya Morogoro, Waziri Kombo leo mara baada ya kumalizika kwa ziara ya kukagua Ujenzi wa Soko Kuu la Kisasa. |
Waziri Jaffo akiwa pamoja katika picha ya kumbukumbu na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Morogoro . |
WAZIRI wa
Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Selemani Jaffo ameipongeza Wakala wa Barabara
za Vijijini na Mjini-TARURA Manispaa ya Morogoro kwa kazi nzuri ya kusimamia ujenzi wa barabara
pamoja na kutengeneza Culvert na mifereji bora yenye kuhimiri nguvu ya maji
wakati wa mvua.
Mh. Jaffo ameyasema hayo leo
Machi 13, 2020 alipokuwa akikagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika
Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro ikiwemo miundombinu ya barabara zilizopo
chini ya TARURA ambapo Ujenzi wa
barabara ya Arc Hotel ni moja ya barabara iliyotembelewa na Waziri Jaffo huku
akiridhika na ujenzi wa mifereji kutokana na ubora na uimara .
Aidha, Waziri Jaffo ametoa
angalizo kwa TARURA kuwa makini katika kuwasimamia wakandarasi wanaojenga
barabara hizo ili ziendane na thamani halisi ya fedha inayotumika.
“ Hizi barabara zetu
tunazijenga kwa gharama kubwa, lakini baada ya miaka miwili tunaweka viraka,
kwa hiyo ni mategemeo yangu barabara hii iwe na uhakika wa miaka 20 na
wakandarasi tunaowapa kazi za ujenzi wa barabara wasiwe wababaishaji, na
nawaagiza TARURA muwabane wakandarasi watutengenezee barabara zenye ubora lakini wahakikishe
kwamba mifereji yote na culvert nazo mzijenge kama mlivyojenga katika barabara
hii kwani hii mifereji ingekuwa dhaifu tungeshuhudia uharibifu mkubwa hapa yote
kwa yote niwapongeze kwa kazi nzuri hamjawahi kuniangusha Manispaa ya Morogoro
mnafanya kazi kwa maelekezo hongereni sana ”Amesema Jaffo.
Katika ziara yake hiyo,
Mh. Waziri amewaagiza Meneja wa TARURA wote nchi nzima kuanzia wa Mikoani hadi
Halmashauri kuhakikisha wanapitai mara kwa mara madaraja na kuyakagua ikiwamo
kusafisha mifereeji inayozibwa kwa mrundikano wa mchanga na matope ili wakati
wa mvua isilete madhara kwa wananchi na kuharibu miundombinu.
Kwa upande wa Meneja wa
TARURA Manispaa ya Morogoro, Mhandisi James Mnene, amemshukuru Waziri Jaffo kwa
pongezi na tamko lake la kutaka fedha zote za matengenezo ya kila siku za
Barabara zitumike katika kuboresha miundombinu ya Mifereji , Culvert pamoja na na madaraja ili kuepusha madhara ya uharibifu wa
miundombinu na madhahara kwa wananchi hususani katika kipindi cha Mvua.
Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI
Mh. Selemani Jaffo, alihitimisha ziara yake kwa
kwa kukagua ujenzi wa Shule ya Sekondari Morogoro baada ya kutembelea
mradi wa Soko kuu la Kisasa linaloendela na Ujenzi katika Manispaa ya Morogoro
Kata ya Mji Mkuu.
Post a Comment