Mkurugenzi Manispaa ya Morogoro afanya ziara ya Kushtukiza Wodi za Washukiwa wa Ugonjwa wa CORONA.
Jengo la Hospitali ya Manispaa ya Morogoro ambalo linaendelea na Ujenzi lililopo Kata ya Mkundi.
Mganga Mkuu wa Manispaa ya Morogoro, Dr. Ikaji Rashid akifungua maji baada ya Wodi hiyo kuwa na uhaba wa Maji na tatizo hilo limekwisha. |
MKURUGENZI
wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba, amefanya Ziara ya kushtukiza katika Wodi za Washukiwa wa Ugonjwa wa CORONA
zilizopo katika eneo la Ujenzi wa Hospitali ya Manispaa ya Morogoro Kata ya
Mkundi .
Ziara hiyo
ya kushtukiza imefanyika leo Machi 31, 2020, ambapo Mkurugenzi ameambatana na
timu ya Wataalamu kutoka Manispaa ya Morogoro akiwemo Mganga Mkuu wa Manispaa
ya Morogoro, Dr Ikaji Rashid pamoja na Muuguzi Mkuu wa Manispaa ya Morogoro, Dr
Assela Kavia.
Aidha, Mkurugenzi amewataka
Wanaohudumia baada ya kupata Wagonjwa waendelee na moyo wa kufanya kazi na kuwa
makini mahala pakazi.
“Najua mpo hapa
kwa lengo la kuwahudumia watu, niwaombe wauguzi msiwanyanyapae endapo kuna wagonjwa
watagundulika kikubwa muendelee kutoa huduma bora katika kuokoa afya za
Wenzenu, hatuombe tuwe na Wagonjwa lakini tahadhari ni muhimu kikubwa kama
Mkurugenzi wenu nimekuja hapa kuona jinsi maandalizi yalivyo nimeridhishwa na
mikakati ya hapa nilisikia maji hakuna lakini leo Mabomba yote yanatoka maji ni
jambo jema sana nipende kuwatakia kazi njema katika mapambano haya ya Virusi
vya Ugonjwa wa CORONA”Amesema
Sheilla.
Post a Comment