Header Ads

Timu ya Wataalamu wa Afya Manispaa ya Morogoro yapiga hodi Makao ya kulelea Yatima ya Mission To The Homeless Children kwa ajili ya kutoa elimu ya kujikinga na Ugonjwa wa CORONA.



Timu ya wataalamu wa Afya Manispaa ya Morogoro wakiwa katika picha ya pamoja na Watoto wanaoishi Makao ya kulelea yatima na watu wenye Mazingira magumu katika Makao ya Mission To The Homeless Chidren Mkundi baada ya kuwatembelea na kuwapa elimu ya kujikinga na Ugonjwa wa CORONA. 

Mratibu wa Ubora wa Huduma za Afya Manispaa ya Morogoro, Dr. Caroline Sakaya (kulia) akiwaonyesha Watoto jinsi ya kusafisha mikono baada ya kunyunyiza dawa kwenye Mikono  katika kujikinga na Ugonjwa wa CORONA, (KUSHOTO), Afisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Morogoro, Sidina Mathias. 
Afisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Morogoro, Sidina Mathias, akimkabidhi dawa Mkurugenzi wa Makao ya Mission To The Homeless Children, Mzee Robert Simba lakini kubwa zaidi Afisa Ustawi amesisitizia Watoto wasitoke nje ya Makao badala yake  wakae sehemu moja ili kujikinga na maambukizi ya Virusi vya CORONA.
Mratibu wa Ubora wa Huduma za Afya Manispaa ya Morogoro, Dr. Caroline Sakaya, akiendelea kutoa elimu ya kujikinga na Ugonjwa wa CORONA kwenye  Makao ya kullelea Watoto Yatima ya Mission To The Homeless Chidren yaliyopo Kata ya Mkundi Manispaa ya Morogoro.
Afisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Morogoro, Sidina Mathias, akiwanyunyizia dawa ya kusafisha mikono Watoto.


Mkurugenzi wa Makao ya Mission To The Homeless Children, Mzee Robert Simba, akisikiliza kwa makini elimu juu ya kujikinga na Ugonjwa wa CORONA.

Watoto wakisikiliza elimu ya kujikinga na Ugonjwa wa CORONA.

Mratibu wa Ubora wa Huduma za Afya Manispaa ya Morogoro, Dr. Caroline Sakaya, akiendelea kutoa elimu ya kujikinga na Ugonjwa wa CORONA kwa Vijana wa Bodaboda pamoja na Bajaji.







No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.