RC Sanare awataka wazazi wabanwe walipe gharama za chakula kwa watoto wao shuleni.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kihonda Maghorofani wakiwa katika Foleni Chakula. |
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba, akitoa utambulisho kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Loata Sanare. |
Mkuu
wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Regina Chonjo , akionja chakula cha Wanafunzi
katika Shule ya Msingi Kihonda Maghorofani.
|
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Loata Sanare amesema Bado kuna
changamoto kubwa ya wanafunzi kupatiwa chakula wakati wa
masomo hali ambayo imechangia wanafunzi wengi kukatisha masomo, kufeli mithiani
yao na ongezeko la utoro .
Kufatia hali hiyo, RC Sanare amezitaka Kamati za Shule kuwabana Wazazi
na walezi wa watoto
wanaosoma madarasa ya awali na shule za
msingi ili waweze kuchangia gharama za chakula cha watoto wao wakati
wakiwa shuleni hivyo kuwasaidia wafanye vizuri kwenye masomo yao na
kuondokana na madhara ya kiafya ikiwemo vidonda vya tumbo
, utoro, wizi na unyanyapaa.
Akizungumza na Kamati ya Shule pamoja na Waalimu, Kamati ya Wazazi
katika Shule ya Msingi Kihonda
Maghorofani pamoja na Watendaji amesema kuwa Manispaa ya Morogoro, imebarikiwa kuwa na chakula kingi lakini
bado shule nyingi hazina huduma ya chakula
shuleni hali ambayo inamkosesha mtoto
haki ya msingi yakupata milo mitatu na hivyo kudhoofisha akili
na mwili.
“Tubadilike wazazi hivi tunajisikia Amani watoto wetu
wanashinda na njaa sisi tunakula , nafikiri wakati umefika sasa wa kuwasaidia
hawa watoto kupata chakula mashuleni kwani ile Shea yake ambayo
angekula akiwa nyumbani ndio atakayokula akiwa shuleni, tuache ubinafsi
tuchangie chakula cha watoto wetu,”amesema RC Sanare.
Amesema kuwa kama wapo
wazazi wanaogoma kuchangia chakula wanakosea sana kwani haiwezikani
mtoto ashinde bila kula chochote tangu asubuhi hadi anaporudi nyumbani
kwani hata makuzi ya mtoto uwezo wa mtoto kuwa kiakili
inategemeana mlo kamili na vyakula mbalimbali vilevile ukuaji wa mwili
kiafya ni muhimu watoto wapate chakula bora ili kujenga kiakili na
kimwili.
Amezitaka kamati za
kukusanya chakula zishirikiane na kamati za wazazi kuhakikisha watoto
wanapata chakula shuleni kwani Mkoa wa Morogoro una chakula kingi
ni aibu watoto kushinda bila kula.
Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Mhandisi
Emmanuel Kalobelo, amesema tatizo la
watoto kutokula shuleni linachangia kufeli kwa wanafunzi kwani wazazi
wengi hawataki kuchangia gharamaya chakula cha Watoto wao hali ambayo
inawafanya watoto wengi kukosa
haki ya kupata chakula wakati wa masomo ingawa
wapo baadhi ya wazazi ambao ujitoa na kuchangia gharama
hizo.
"kukosekana chakula kunamuathiri mtotoanakuwa
siyo msikivu ana kosa raha , pia inavuja morali ya kufundisha kwa
mwalimu kwani huwezi kufundisha watoto wakiwa na njaa , hata ukitoa zoezi
watoto hawatafanya hivyo ni muhimu wazazi na viongozi
wa shule wakae na kujadili namna ya kumsaidia mtoto kupata
mlo shuleni kwani wapo wanafunzi wanaotoka kwenye familia maskini
hivyo kutolewa kwa chakula shuleni kunawasaidia kupata japo milo
miwili kwa siku hivyo kufanya vizuri kwenye masomo yao."amesema RAS
Kalobelo.
Katika hatua nyengine, Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe.
Regina Chonjo, amesema kutotolewa kwa chakula mashuleni kunawanyima
wanafunzi haki ya kusoma na kufanya vizuri kwenye masomo
kwani utakuta wanawaza chakula badala ya masomo na
kujisikia vibaya pindi wakiwaona wenzao wanavyokula na wengine ujikuta
vichwa vikiwauma kutokana na kutokula.
kwa upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, mhe.
Pascal Kihanga, amesema pamoja na
jitihada mbalimbali zilizofanywa na uongozi wa shule hiyo
kuwashawishi wazazi watoe pesa
za chakula lakini wanagoma ni wazazi wachache ndio wanaona umuhimu na
kulipia gharama hizo nashindwa kuelewa sijui tatizo lipo wapi labda
hali ya uchumi ni mbaya au mwamko mdogo kwani ni
25% ya wanafunzi ndio wanaopata chakula shuleni.
Post a Comment