Picha mbalimbali zikionyesha matukio tofauti tofauti katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyoandaliwa na Manispaa ya Morogoro kwenye Uwanja wa Mpira wa Jamhuri Machi 8, 2020.
| Watumishi wa Manispaa Morogoro wakiingia uwanjani baada ya maandamano . |
| Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro, Eng. Emmanuel Kalobelo, akikata keki. (kulia) Afisa Maendeleo ya Jamaii Manispaa ya Morogoro, Enedy Mwanakatwe. |
| Watumishi wa Manispaa Morogoro wakiingia uwanjani baada ya maandamano . |
| Mkurugenzi wa Manispaa Morogoro, Sheilla Lukuba akisakata ngoma na Msanii wa Singeli Snura Mushi. |
| Msanii wa Singeli Snura Mushi akiwa na Afisa Uchaguzi wa Manispaa ya Morogoro Pendo Chagu wakionesha uhodari wa kutumbuiza. |
| Waheshimiwa Madiwani Manispaa ya Morogoro wakivutana kamba na Watendaji wa Manispaa ya Morogoro na kufanikiwa kuibuka washindi. |
| Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba, akiwa jukwaani pamoja na Msanii wa Singeli Mzee wa Bwax. |
| Keki iliyoandaliwa kwa ajili ya kusherekea Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani. |
| Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga akitoa neno. |
| Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba, akionesha kufurahishwa na maadhimisho hayo. |
Post a Comment