MANISPAA YA MOROGORO YAADHIMISHA MIAKA 63 YA UHURU WA TANGANYIKA
MANISPAA ya Morogoro imeadhimisha miaka 63 ya Uhuru wa Tanganyika kwa kufanya mdahalo kuhusu maendeleo yaliyopatikana katika kipindi hicho.
Sherehe hizo za uhuru zimefanyika Desemba 09-2024 katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi Kuu ya Manispaa ya Morogoro na kuhudhuriwa na wazee marufu pamoja na wananchi.
Akizungumza katika mdahalo huo, Mkuu wa Wilaya ya Morogoro,Mhe. Mussa Kilakala, amesema kwa heshima ya mafanikio haya ya kihistoria, Serikali inafuatilia sekta zake kwa kutaja mafanikio yake, matatizo na changamoto ilizozikabili tangu Uhuru na kupanga mwelekeo wa baadaye.
Manispaa ya Morogoro imepata mafanikio mbalimbali ikiwemo sekta ya kilimo ambapo kipindi cha miaka 63 (1961-2024) Sekta ya kilimo imekuwa na ongezoko la chakula cha kutosha huku uzalishaji wa kwa hekta kwa mazao imeongezeka ambapo tani 1 mwaka 2015/2016 hadi kufikia tani 2.3 mwaka 2023/2024 na uzalishaji wa mazao bustani uliongezeka kutoka tani 5 mwaka 2025/2016 hadi tani 16 mwaka 2023/2024.
Upande wa Sekta ya Viwanda, umeimarika kwa kushirikiana Serikali na Sekta binafsi ambapo mwaka 1961 hakukuwa na kiwanda kikubwa na vya kati na sasa 2024 viwanda vikubwa vipo 10, viwanda vya kati 5 na viwanda vidogo 452.
Sekta ya Umeme, mwaka 1961 maeneo mengi hayakuwa na umeme wa Gridi ya Taifa, ambapo katika kipindi cha miaka 63 maeneo mengi yamepatiwa umeme ambapo kwa Manispaa zaidi ya Mitaa 271 imesambazwa umeme.
Upande wa elimu msingi na Awali, Elimu ya Awali na Msingi, miaka ya 1975 Manispaa ya Morogoro ilikuwa na shule 8 za Serikali na mwaka 2024 ina jumla ya shule za Msingi 128 kati ya hizo Shule za Serikali ni 75 na binafsi ni 53.
Viwanda vikubwa vipo 10, viwanda vya kati 5 na viwanda vidogo 452.
Mwaka 2024 shule za Sekondari 60 ambapo 30 za Serikali na 30 shule binafsi,mashirika ya dini au Taasisi ,mwaka 1961 kulikuwa na wanafunzi 163 na mwaka 2024 wanafunzi wameongezeka kufikia 28476.
Huduma za Afya, mwaka 1961 Manispaa haikuwa na hata kituo kimoja cha kutolea huduma za afya, kwa sasa Manispaa ina jumla ya vituo vya kutolea huduma za afya 87 ambapo kuna Hospitali 4 vituo vya afya 14 na Zahanati 54 ,Kliniki 15 na Maternity home
Sekya ya uvuvi ina jumla ya masoko 2 ya Samaki , mabwawa ya samaki 175,kutoa elimu ya ufugaji kwa zaidi ya watu 652.
Kwa mwaka 2020/2021 katika Sekta ya uvuvi,makusanyo ya mapato yalikuwa 72,357,500.00 hadi kufikia 2023/2024 makusanyo yalipanda kufikia 139,199,700.00
Post a Comment