MKURUGENZI MANISPAA YA MOROGORO AGAWA NDOO ZA MAJI KATIKA MAKAO YA KULELEA WATOTO PAMOJA NA WAZEE WASIOJIWEZA KWA AJILI YA KUJIKINGA NA UGONJWA WA CORONA.
Mlezi wa Mkao ya Raya, akiwa pamoja na Watoto , akionyesha ndoo aliyokabidhiwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro kwa ajili ya kunawia katika mapambano ya Virusi vya CORONA. |
Makabidhiano ya ndoo katika Makao ya Mehayo yanayolea Watoto wenye ulemavu pamoja na utindio wa Ubongo yaliyopo Kata ya Mazimbu. |
Makabidhiano ya ndoo katika Makao ya Agape Children's Village. |
Makabidhiano ya ndoo katika Makao ya Dar-Ul- Muslimeen Kata ya Mbuyuni. |
MKURUGENZI wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba, amevigawia
jumla ya Vituo 7 vya Makao ya Kulelea
Watoto yatima na wanaoishi katika Mazingira magumu pamoja na Wazee wasiojiweza
ndoo za kunawia , sabuni pamoja na mabeseni ya kukingia maji machafu kwa ajili
ya kujikinga na Ugonjwa wa CORONA.
Akizungumza na kukabidhi ndoo hizo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya
Morogoro, Afisa Ustawi wa Jamii Manispaa
ya Morogoro, Sidina Mathias, amesema ndoo hizo alizo zitoa Mkurugenzi ni moja ya jitihada za kuunga Mkono Serikali
kwa ajili ya mapambano dhidi ya Ugonjwa wa CORONA .
Amesema kuwa, kwa kutambua umuhimu wa Makao hayo ya Watoto
wanaoishi katika mazingira magumu pamoja na Wazee wasio jiweza , Mkurugenzi
ameona ni bora kuwapelekea ndoo ili zile pesa wanazopata Makao hayo ziweze
kuwasaidia katika matumizi ya huduma nyengine.
“Leo tuna toa ndoo hizi kwa Makao ya kulelea Watoto yatima,
wanaoishi katika mazingira magumu pamoja na Wazee wasiojiweza, Mkurugenzi wetu
kwa kutambua makundi haya yaliyopo katika Manispaa yake, ameona ni vyema
akayakumbuka kwa kuyapatia ndoo za kunawia mikono, mabeseni pamoja na sabuni za
kunawia katika kipindi hiki cha mapambano dhidi ya Virusi vya CORONA, amekuwa
akishirikiana vyema na makundi haya katika kutoa misaada mbalimbali pamoja na
huduma lakini hili alilolifanya leo ni jambo jema katika kuhakikisha wananchi
hawa wanakuwa salama dhidi ya Ugonjwa huu”Amesema Sidina.
Kwa upande wa Mfawidhi wa Makao ya Wazee wasiojiweza Funga funga, Bi.Rehema Kombe, amemshukuru
sana Mkurugenzi wa Manispaa kwa jitihada zake za kuwajali Wazee hao.
“Tunamshukuru sana Mkurugenzi wetu, ameonyesha ni jinsi gani
anavyojali afya za Wananchi wake, nakumbuka hii sio mara ya kwanza kutusaidia
katika Makao yetu , alishawahi kutupatia TV pamaoja na King’amuzi kwa gharama
zake na upendo wake, kikubwa tunazidi kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ambariki kwa
kile alichokitoa hakika tumepata Mama anaye tujali, kwa kutambua mchango wake
pongezi hizi hazitaishia kwa maneno pekee bali tutamwandikia barua ya shukrani
kwa jinsi anavyozidi kujitoa na kuonyesha upendo kwetu na kuwatia faraja Wazee
hawa”Amesema Kombe.
Naye, Mlezi wa Makao ya Mgolole, Sister Palagia Maria , amesema alichokionyesha Mkurugenzi
ni upendo kwa Watoto na kuwajali katika afya zao dhdi ya mapambano ya Virusi
vya CORONA.
“Mkurugenzi wetu amekuwa akijitoa sana, hivi karibuni
akiambatana na Mkuu wa Wilaya wa Morogoro
Mhe. Regina Chonjo , walishawahi kuja hapa wakatupatia msaada wa Vyakula
,hivyo huu ni mwendelezo wa kutuunga mkono na tunamuomba aendelee kututhamini
na kutusaidia asichoke yeye ni Mama yetu tunapokwama anatakiwa atukwamue, hiki
sio kidogo amejinyima na familia yake na kuja kutuletea hapa tunampongeza sana
na kumtakia majukumu mema ya kazi zake na kuifanya Manispaa yetu kupiga hatua
zaidi za Maendeleo”” Amesema Sister Parakia.
Naye Mwenyekiti wa Wazee
hao, Mzee Joseph Kaniki, amemshukuru Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro kwa
kuwajali na kuwathamini katika kipindi hiki cha mapambano ya Virusi vya CORONA.
Katika hatua nyengine, Sidina, amesema huu ni mwanzo , hivyo
Mkurugenzi amejipanga na timu yake ya Wataalamu wa Afya kwa kushirikiana na
Uongozi wa Wilaya ya Morogoro, chini ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhe. Regina Chonjo
kuhakikisha elimu ya kujikinga dhidi ya maambukizi ya Virusi vya CORONA
inatolewa kila kona katika kulinda hali za afya za Wananchi wao.
Miongoni mwa Makao yaliyopatiwa ndoo, sabuni na mabaseni ni
pamoja na Makao ya kulelea Watoto Mgolole, Makao ya kulelea Wazee wasiojiweza
Funga funga, Raya, Agape Children’s Village, Dar-Ul- Muslimeen , Mission To The
Homeless Children.
Post a Comment