Header Ads

Watembea uchi kukiona cha mtema kuni:DC Mjema





MKUU Wa Wilaya ya Ilala, Mh Sophia Mjema, amemuagiza OCD kuhakikisha anawakamata Wasichana  wote wanaovaa nusu uchi.

Amesema haipendezi Taifa kama Tanzania Vijana Wa Kike  wakipoteza utamaduni wao na kuiga utamaduni Wa nje huku akisema ni jambo baya  kwa Taifa hili.

 "  ifike wakati tuwe wakali kwa watoto wetu, tuwafundishe  wavae vizuri lakini  wakuwarekebisha ni  sisi wazazi sasa kama wazazi hamuwezi sisi tutawarekebisha kwa lazima na kuwachukulia hatua" Amesema DC Mjema.

Aidha amesema nchi hii ina  utamaduni na desturi zake , hivyo lazima tuulinde utamaduni wetu kwa maslahi mapama ya Taifa letu na kizazi chetu.

 Mbali na watembea nusu uchi, pia amepiga marufuku wadada wanaofanya ngono zembe (Madada  poa) kwamba waache Mara moja tabia hiyo.

Aidha amesema ili kupinguza tabia hiyo ni lazima tuhakikishe wale wanao watumia wanaacha tabia hizo,  kwa kufanya hivyo tutapunguza tatizo hilo.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.