Header Ads

DC Mjema atoa agizo kwa OCD kuwasweka ndani wavamizi Wa Kiwanja cha Bi Tausi Kata ya Buyuni.







 MKUU Wa Wilaya ya Ilala, Mh Sophia Mjema, amemtaka OCD kwa kushirikiana na Afisa Ardhi kuhakikisha wanawakamata wote  waliohusika na uvamizi Wa Kiwanja cha Bi Tausi Kata ya Buyuni.


 Agizo hilo  amelitoa Leo Oktoba 2/2019 kwenye ziara yake  aliyoifanya Kata ya Buyuni katika kusikiliza kero za Wananchi.


Akizungumza mbele ya Wananchi, amesema kukamatwa kwa wavamizi hao kutapunguza uvamizi Wa viwanja.

Amesema wimbi la  uvamizi Wa Viwanja hususani maeneo ya Pembezoni mwa Ilala yamekuw makubwa hivyo wahusika wakikamatwa itakuwa fundisho kwa wengine.

 " OCD hakikisha Kesho na Afisa Ardhi mfike eneo hilo  la Bi Tausi , kama wamejenga bomoeni na muwakamate, yule bibi ni mbovu Wa miguu namjua hivyo mjitahidi kumpa ulinzi" Amesema DC.

 Aidha amesema kuwa kwakuwa taarifa zake anazo basi wataangalia uwezekano Wa kumsamehe kodi ya pango kulingana na Sheria inavyosema.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.