Mkurugenzi Manispaa Morogoro Mjini, Sheila Lukuba, afanya ziara ya kukagua vituo vya zoezi la uandikishaji wapiga kura
MKURUGENZI wa Manispaa ya Morogoro, Mh Sheila Lukuba, amefanya ziara yake ya kwanza ya kutembelea vituo vya Uandikishwaji wa zoezi la upigaji kura tangia ateuliwe kuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro na Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli.
Ziara hiyo ameifanya Leo Oktoba 8/2019 alipotembelea baadhi ya vituo ili Kuona hali halisi ya zoezi hilo linavyoendelea.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, amesema lengo la ziara hiyo ni Kuona taratibu zinafuatwa kwa makalani na mawakala wa vyama vya siasa, pamoja changamoto zinazojitokeza.
Aidha amesema zoezi ni zuri lakini kikubwa amewahamasha watumishi wajiandikishe kwani ni haki yao ya kikatiba.
Miongoni Mwa vituo alivyotembelea ni pamoja naShule ya msingi nguzo, Kituo cha Mwande kilichopo kata ya Mchangani, Kihonda Mbuyuni na Kata yw Kihonda.
" Nimeanza ziara hii fupi lakini hatujatembelea vituo vyote ila tumechagua vichache na japo kuna changamoto ndogo ndogo tumezitatua hivyo tunategemea zoezi hilo litakwenda vizuri" Amesema Mkurugenzi.
Naye Msimamizi wa Uchaguzi , Manispaa ya Morogoro, Ndugu Waziri Kombo, amesema kuna jumla ya vituo 294,ambapo jumla ya Wananchi Lak 1 na 77 elfu wanatarajia kujiwndikisha na kupiga kura.
" Tumeridhishwa na zoezi hili, tangia tuanze kukagua masaa machache lakini tunaona namba ya watu inaridhisha, matumaini yetu tulichokidhamiria kitafanyika na malengo yetu yatakuwa mazuri licha ya changamoto ndogo ndogo zilizojitokeza" Amesema Kombo.
Aidha ametoa agizo kwa wasimamizi wa vituo kuwa kama wanabadilisha Kituo wawashirikishe Wananchi wao na kama kuna changamoto waseme mapema kabla ya kutokea madhara.
Amewaomba wananchi wajitokeze kwa wingi kujiandikisha ili waweze kuwapata viongozi watakaowaletea maendeleo.
Kwa upande wa Mwananchi, Janeth mwaijonga ameomba Wananchi wajitokeze ili waweze kupiga kura. Pia amesema wanahitaji vuongozi bora wenye uwezo Wa kuwasaidia matatizo yao.
Post a Comment