Meya Mstaafu Ilala akunwa na ziara ya DC Mjema, afunguka mazito juu ya kujihudhuru nafasi yake na kujiunga CCM.
WAKATI ziara ya Mkuu Wa Wilaya Ilala Mh Sophia Mjema ikiendelea, aliyekuwa Mstahiki Meya Manispaa ya Ilala Mh Charles Kuyeko, amefunguka mazito huku akimpongoza DC Mjema kwa kazi kubwa anayoifanya ya kumsaidia Mh Rais Dkt John Magufuli katika kutatua Kero na kuwaletea Wananchi Maendeleo.
Hayo ameyasema Leo Oktoba 3/2019 wakati Wa ziara ya DC Mjema Kata ya Bonyokwa. Aidha mbali na kumpongeza ametoa siri ya kujihudhuru nyadhifa yake ya Udiwani pamoja na Umeya , ambapo amesema Chama cha CCM ndicho kilichomlea na kumfikisha alipo licha ya kutumikia upinzani kwa tiketi ya CHADEMA.
Amesema awali kabla ya kujiunga na CHADEMA , aliwahi kuwa miongoni mwa wanachama Wa mwanzo Wa CCM walipata kadi miaka ya 1974 baada ya Munganiko Wa Afroshiraz na TANU.
Aidha, amesema kujitoa kwake CCM mwaka 2014 kulitokana na wimbi la wanachama Wa CCM kutokumkubali aliyekua mgombea mteule Wa CCM udiwani mwaka 2015, ambapo hapo ndipo wanachama wakamwambia atafute chama chengine cha upinzani na ndipo alipoenda CHADEMA wakampitisha kuwa mgombea wao akafanikiwa kuwa Diwani na kupata kura za kishondo na kuwa Mstahiki Meya Wa Ilala.
" Mimi nilikuwa CCM, ndiye niliyekuwa mgombea niliyekubalika na wanachama Wa CCM, lakini baada ya mwenezi Ilala kumleta mgombea wake basi wanachama wakanishauri niende upinzani wakanifuata nikashinda" Amesema Kuyeko.
Pia amesema wakati anawaita Wananchi kukaa vikao walikuwa wakaidi wakidai hafanyi kazi , kwa Kuona hayo akaona ni vema arudi nyumbani kuungana kwa ajili ya kuwaletea Wananchi Maendeleo.
Amesema watu watoe dhana ya yeye kuutaka udiwani mwakani, kwani hata alipoachia ngazi hakutaka kugombea aliacha nafasi hiyo kugombewa na wengine.
" Niwatoe hofu Ndugu zangu, Mimi sio mroho Wa madaraka, uongozi ni kuachiana vijiti, ningekuwa nataka madaraka ningegombea tena lakini sikufanya hivyo, itakapotokea Chama changu kikaniteua nigombee nitagombea au Serikali ikinipa kazi nyengine nitafanya , shida yangu ni Kuona watu wanapata Maendeleo.
Amesema anaimani kubwa na Rais Wa awamu ya tano, Mh Rais Dkt John Magufuli, Yale waliyokusudia wapinzani anayafanya kwa vitendo , hivyo amewataka watu waachane na siasa uchwara wamuunge mkono ili miradi mikubwa imalizike na kulifanya Taifa hili lipige Maendeleo.
Post a Comment