DC Mjema afufua matumaini ya ukarabati Soko Ilala.
MKUU wa Wilaya Ilala Mh Sophia Mjema amefufua matumaini ya ukarabati wa Soko la Ilala Mara baada ya kupokea changamoto zinazoikabili Soko hilo kutoka kwa Viongozi.
Matumani hayo ya kuendelea na ukarabati wa soko hilo, yametokana na utatuzi wa changamoto ya bei ya vifaa vya ujenzi na kukosekana kwa wasambazaji wa Vifaa ( Supplier) wanaoendana na bajeti iliyotengwa.
A
idha DC Mjema ameitaka kamati inayohusika na ujenzi kupitia Uongozi wa Kata waachane na vifaa vya gharama badala yake waongee na Kampuni ya vifaa vya ujenzi ya Beijing New Building Materials kwa ajili ya kupata vifaa vyenye thamani ndogo.
" Mradi umechelewa sana , niwaombe tuanze kufanya kitu, hizi siku mbili zilizobakia, nendeni Beijing new Building muwaambie mkuu wa Wilaya katutuma, pale mtapata Saruji pamoja na vifaa vyengine kwa bei ya chini , huu ni ukarabati na sio ujenzi haiwezekani tutumie pesa nyingi kama tunajenga wakati tunafanya ukarabati " amesema Mjema.
Hata hivyo DC Mjema amesema kuwa baada ya kupata bei nafuu ya vifaa wahakikishe wanafuata taratibu na Sheria za kutoa pesa hiyo kwani pesa za Serikali zina utaratibu wake katika matumizi .
Naye Mwenyekiti wa kamati ya Maendeleo na Diwani wa Kata ya Ilala, Mh Saadi Khimji, amesema ujenzi huo ulisainiwa Oktoba 15 mwaka 2019, lakini cha kushangaza mpaka sasa hakuna kilichofanyika.
Amesema kuwa Manispaa ya Ilala ilitenga milioni 74 , kwa ajili ya ukarabati huo lakini kikwazo kikubwa kilichokwamisha ni kutosimama vizuri kwa Mhandisi wa mradi huo.
Amesema mhandisi anayesimamia mradi huo amekua katika mkanganyiko kwani katika pesa ya wasambazaji wa bati moja walitenga Shilingi Elfu 26 badala ya 28 hadi 29 elfu , na upande wa saruji walitenga elfu 14 pekee bila gharama za usafirishaji kitu ambacho kimefanya mradi huo kuchelewa.
Miongoni mwa maeneo yaliyopewa kipaumbele katika ukarabati huo ni pamoja na eneo la wauzaji nyanya, eneo wauza Kuku, matenga pamoja na mama lishe.
Post a Comment