Mkurugenzi Manispaa Morogoro atangaza uuzwaji wa Viwanja 600
MKURUGENZI wa Manispaa Morogoro, Mh Sheila Edward Lukuba, ametangaza kuvipiga bei Viwanja 600 vilivyopo katika Manispaa yake. Tangazo hilo amelitoa leo Oktoba 23 mwaka 2019.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, amesema Viwanja hivyo vimepimwa na vipo katika maeneo ya mitaa ya Kiegeya B Kitalu "BB".
Amesema Mwananchi yeyote atakaye hitaji kiwanja, afike Ofisi ya Mipango Miji kwa ajili ya ununuzi wa fomu za Viwanja ambapo fomu hizo zitaanza kuuzwa tarehe 14, Oktoba, 2019 hadi tarehe 14, Novemba, 2019.
Amesema fomu ya bei moja shilingi elfu 20,000/= kwa Viwanja vya ujazo wa juu na chini vya matumizi ya makazi na Biashara.
Amesema kwa kila mita moja ya mraba Viwanja vya makazi shilingi 4000/= na vya biashara shilingi 4500/=.
Pia amesema muda wa malipo ni miezi 2, ambapo ndani ya mwezi mmoja Mteja atalipa nusu gharama Kiwanja.
" Hii ni fursa tunawaomba Wananchi mchangamkie fursa hii na mjitokeze kwa wingi, na malipo yote yatalipwa kupitia akaunti za Benki zitakazo ainishwa katika Ankara ya malipo na Mteja atapaswa kuwasilisha nakala ya malipo ya Benki ( Pay Slip) ili apatiwe stakabadhi ya Manispaa " Amesema Mkurugenzi.
Pia amefafanua kwamba ,Mteja atakaueshindwa kukamilisha gharama za kiwanja baada ya Mirza miwili , Ofisi italazimika kuuza kiwanja hicho kwa Mteja mwengine bila taarifa zaidi kwake na fedha zake zitareneshwa baada ya makato ya asilimia 20.
Post a Comment