DC Mjema amtaka Meneja mpya Soko la Samaki Feri kujipanga katika kutatua kero za wafanya biashara hao.
MKUU wa Wilaya Ilala Mh Sophia Mjema , amemtaka Meneja Mpya wa Soko la Samaki Feri kujipanga na Timu yake ili Kuona uwezekano wakuzitatua kwa haraka kero za wafanya biashara hao.
Hayo ameyasema Leo Oktoba 9/2019 ,ikiwa ni ziara yake ya kutatua kero za Wananchi katika Manispaa ya Ilala.
Amesema amepokea Changamoto nyingi lakini kubwa ikiwamo baadhi ya wafanya biashara kuingiliana majukumu katika Kanda zao za biashara kitu ambacho amekipinga vikali.
" Nimesikia kuna mwingiliano wa zone zenu za biashara, namuagiza Meneja nenda kakae uandike vibao vinavyo onyesha mipaka ya zone na biashara zake ili kukwepa muingiliano wa kibiashara atakaye kiuka mchukulie hatua" Amesema Mjema.
Amesema ni jambo jema Kuona miradi iliyoahidiwa na Mh Rais Dkt John Magufuli imefikia 90%.
pia amefurahishwa kuwepo kwa Red Cross ( hudua ya kwanza), huku akisema huduma hiyo itasaidia sana wakati wa kutokea Janga la moto na kuokoa Mali na bidhaa za wafanya biashara hao.
Pia amemuagiza Meneja wa Soko hilo ,kuhakikusha anakaa na wafanya biashara wake wanao miliki vyombo vya moto ili kuona jinsi ya kutatua kero zao juu ya kulipishwa tozo za egesho ( Parking).
Kuhusu mama lishe zone namba 5 kuwe kewa geti , DC Mjema amesema Uongozi wa Soko hilo ukae UDART waone jinsi wanavyoweza kuyaweka sawa ili Kuona jinsi gani pande zote mbili zinaweza kuwa salama na kukwepa uharibifu utakaojitokeza.
Naye Mkuu Wa Soko la Samaki Feri , Ngugu Dennis Mrema, amesema maagizo yote atayafanyia kazi.
Post a Comment