Header Ads

DC Mjema awatangaza vita dhidi ya wapotoshaji zoezi la uandikishaji wapiga kura.









 MKUU wa Wilaya ilala Mh Sophia Mjema amesema hatowakalia macho wanaopotosha zoezi la uandikishaji daftari la wapiga kura.

Hayo ameyasema Leo Oktoba 11/2029 wakati wa kufanya ziara ya kukagua vituo vya uandikishaji wapiga kura katika maeneo tofauti tofauti katika Manispaa ya Ilala.

Akizungumza na waandishi wa Habari, amesema wapo katika upelelezi wa kuwabaini wanaofanya vitendo hivyo na endapo watawakuta na makosa hayo watachukuliwa hatua Kali za kisheria.

" Nimepata malalamiko hayo na tayari nimewatuma watu wangu , tukiwakata tunawachukulia hatua Kali za kisheria ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hizo" Amesema Mjema.

Aidha, amesema Kitambulisho cha kupiga kura hakitatimika bali  kinachotakiwa ni majina kamili .

Hivyo, amewataka Wananchi wajitokeze kwa wingi kwani zoezi hilo litaisha Oktoba 14 na hakuna muda wa nyiongeza utakaowekwa.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.