DC Mjema aagiza TAKUKURU kuwashughulikia Viongozi waliouza maeneo kinyume na Sheria.
MKUU Wa Wilaya Ilala Mh Sophia Mjema, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa ( TAKUKURU) , kuhakikisha wanawakamata haraka sana Baadhi ya Viingozi wanaoguswa na kashfa ya uuzaji maeneo kinyume na Sheria.
Ameyasema hayo leo Oktoba 2/2019 Mara baada ya kuhitimisha ziara yake aliyoifanya kwenye Kata ya Buyuni, Pugu Stesheni pamoja na Pugu Kajiungeni.
Akizungumza na Waandishi Wa Habari, amesema maeneo yote yaliyoko pembezoni Mwa Ilala yamekuwa yakiongoza kwa migogoro ardhi lakini wasababishaji wakubwa ni baadhi ya viongozi wao walioko kwenye Kata zao pamoja na Mitaa yao.
" TAKUKURU pamoja na OCD mkishirikiana na Afsa Ardhi fuatilieni haya malalamiko , wapo baadhi ya viongozi wanatajwa tajwa sasa kabla sijamaliza ziara zangu nataka Kuona matokeo ili kesi hizi tuzimalize zimekua sugu sana hususani maeneo haya ya Chanika, Pugu, Buyuni, na maeneo yote ya pembezoni Mwa ilala" Amesema DC.
Aidha, amesema Rais Dkt John Magufuli, amekuwa akipambana sana kuhakikisha awamu hii ya tano changamoto zote za migogoro ya ardhi inapungua na kumalizika kabisa lakini bado ameshangaa Kuona baadhi ya Watendaji hawataki kwenda na kasi ya Awamu ya tano.
Amesema Serikali hii ina lengo la kuhakikisha ifikapo mwakani kabla ya uchaguzi kero zote na miradi yote iwe imekamilika ili Rais Dkt John Magufuli aweze kufikilia vitu vikubwa zaidi vya kupelekea Taifa hili Maendeleo zaidi badala ya kurudi nyuma.
Amesema lengo la ziara zake ni Kuona kero za Wananchi zinapungua na kuisha kabisa , hivyo yale yaliyojitokeza wanayachukua na kwenda kuyafanyia kazi ili kuendana na kasi ya Mh Rais Dkt John Magufuli pamoja na kumuunga mkono kwa kazi kubwa anazofanya katika kuwaletea Maendeleo Wananchi wake.
Katika hatua nyingine, amewaonya Wenyeviti Wa mitaa kuacha Mara moja tabia za kujihusisha na uuzaji Wa Viwanja kihorera ili kupunguza wimbi la wavamizi na migogoro ya ardhi inayotokea kwa Wananchi.
Post a Comment