Header Ads

DC Mjema ataka miradi yote itekelezwe kwa wakati na Kuonyesha thamani ya fedha iliyotumika.






MKUU wa Wilaya Ilala Mh Sophia Mjema, amewataka Wasimamizi wa miradi kuhakikisha miradi yote inatekelezwa kwa wakati pamoja na kuonesha thamani ya pesa iliyotumika.


Hayo ameyasema Leo Oktoba 15/2019 katika ziara iliyofanyika kata ya  Minazi Mirefu,  ikiwa ni kata ya 20 tangia aanze ziara zake za kutatua kero za Wananchi katika Wilaya ya Ilala.

Akizungumza na waandishi wa Habari, amesema kukamilika kwa miradi kwa wakati kunasaidia kutoa huduma iliyokusudiwa mapema kwa Wananchi.

Amesema kuwa, kama kuna viashiria vya kukwama kwa mradi , wasimamizi wa miradi hiyo wanatakiwa kuwasiliana na Ofisi yake  kuliko kukaa kimya.


 " Ipo  miradi inayokwama kwa sababu ya uzembe au ufisadi lakini mingine ni kukosa mawasiliano na kutokushirikishwa, wasimamizi jitahidini kutupatia taarifa pale mnapokwama mtuambie, miradi hiyo ni pesa za Wananchi,  hivyo mkiikwamisha hatueleweki kwa wakubwa zetu"  Amesema Mjema.


Mbali na kusikiliza kero, lakini amepata nafasi ya kuutembelea mradi wa Soko la  kisasa kata ya Minazi mirefu, wenye thamani ya Shilingi Milioni 600.

Naye Msimamizi wa Mradi huo wa Soko, unaotekelezwa kupitia na Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, chini ya uboreshwaji wa miundombinu Mkoa wa Dar Es  Salaam ( DMDP),  Mhandisi John Maguli, amesema mpaka sasa ujenzi huo umetumia   Milioni 200 imeshatumika.

Amesema mradi huo ulitakiwa kukamilika Oktoba 31 mwaka huu, lakini suala la ucheleweshwaji fidia ulichangia kuchelewa kwa mradi huo.


" Tuna mshukuru  mama yetu Mkuu Wa Wilaya Ilala Mh Sophia Mjema kwa kuutembelea mradi huu  ili kujua Maendeleo yake  , kwa kweli mradi unaendelea vizuri, tulipanga mradi huu ukamilike Oktoba 31 mwaka huu, lakini tunaomba tuongezewe muda kwani ucheleweshwaji wa fidia umechangia kuchelewa kuanza mradi" Amesema Maguli.

 Pia amesema katika fidia, jumla ya Wananchi 42 wameshalipwa fidia, na mradi huo ukikamilika unategemea kuchukua jumla ya Wafanyabiashara 200.

  Katika hatua nyengine, Diwani wa kata ya Minazi Mirefu , kupitia tiketi ya Chama cha Wananchi ( CUF), Mh Kassimu Mshamu, ameipongeza Serikali ya awamu ya tano, chini ya Rais Dkt John Maguli , kwa Utekelezaji wa miradi mikubwa ikiwamo ujenzi w Soko hilo, bara bara kiwango cha lami, utoaji wa mikopo isiyo na riba kwa vikundi vya ujasiriamali.


" Tumefurahi kupata ugeni huu katika kata yetu, tuna ipongeza Serikali kwa ujenzi wa Soko hili, tunaimani utatoa ajira kwa Wananchi na wakazi wetu, pia ujenzi wa bara bara kiwango cha lami umeturahisishia kero za usafiri, pia vikundi vya vyetu vya walemavu wamepewa Bajaji 10 , tunashukuru sana" Amesema Diwani Mshamu.

 Pia Amesema  hawana Zahanati ya kata kutokana na ufinyu wa eneo na nyumba nyingi zimebanana. Mbali na Zahanati, amesema hawana Shule ya Msingi mpaka walipe fidia kwa maeneo.

Pia amesema wazee wengi wamekosa huduma ya kadi za matibabu.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.