Header Ads

DC Mjema atoa agizo TAKUKURU kuchunguza Mradi wa Kituo cha Afya Kata ya Mzinga.





 MKUU wa Wilaya Ilala Mh Sophia Mjema, ameiagiza TAKUKURU kumfuatilia aliyekuwa mhandisi wa mradi wa Kituo cha Afya Kata ya Mzinga ili kuona matumizi halisi ya ujenzi wa mradi huo, hii ni kutokana na  kutoridhishwa na pesa iliyotumika ya Shillingi Milioni 120 mpaka sasa .

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Oktoba 10/2019, amesema pesa iliyotumika ni kubwa sana na ujenzi hauja kamilika .


 Amesema mhandisi huyo ametumia pesa nyingi na ameingiza Serikali hasara, hivyo ni lazima hatua za uchunguzi zichukuliwe  kabla ujenzi haujaendelea.

 Amesema kwa taarifa  aliyopewa imeonesha gharama iliyotumika hadi sasa  ni Shilingi Milioni 120 jambo ambalo amelipinga vikali.

" Huu sio uzalendo, hatua iliyofikia haoendani na thamani ya pesa , pesa ni kubwa mno, TAKUKURU nakuagiza Fanya uchunguzi na watupatie thamani ya kila kifaa kilichotumika na ikigundulika amekula pesa ataitapika na tutamchukulia Sheria Kali " Amesema Mjema.

Aidha amesema kuwa ujenzi huo asipewe tena huyo mhandisi hadi  atakapokamilisha Yale maamuzi waliyoyatoa na kuonesha  thamani halisi ya vifaa vilivyotumika.

 " Pesa hizi ni za kodi yetu, Rais wetu Dkt John Magufuli anataka Maendeleo , hivyo kama unapatiwa mradi hakikisha unatumia pesa kulingana na thamani halisi ya ujenzi na sio kujilimbikizia pesa huku Wananchi wakibakia kutoa lawama kwa Serikali yao kwa madai ya miradi kutokukamilishwa kwa wakati" Ameongeza DC Mjema.

 Pia amepata nafasi ya kutembelea miradi kadhaa inayoendelea ikiwamo mradi wa Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Mzinga wenye thamani ya Milioni 51 ambapo Manispaa imetoa Milioni 35 na Nguvu za Wananchi Milioni 16, mradi wa Kituo cha Polisi Mzinga pamoja na mradi wa Ofisi ya Kata ya Mzinga ambacho kinategemewa kutumia gharama ya Shilingi Milioni 150 hadi  ujenzi huo ukamilike.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.