Header Ads

DAS ILALA AANGIZA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KULIPA KODI KWA WAKATI ILI KUTEKELZA MIRADI MBALIMBALI.








 KATIBU Tawala Wa Wilaya ya Ilala, Sheila Edward Lukuba, amewataka wafanyabiashara Wa Kariakoo kulipa kodi kwa wakati ili miradi ya maendeleo imalizike kwa wakati.


Hayo ameyazungumza Jana Mara baada ya kukamilika kwa ziara ya Mkuu Wa Wilaya ya Ilala Mh Sophia Mjema iliyofanyika Kata ya Kariakoo Kaskazini Leo Oktoba 1/2019. Aidha amesema kuwa Mh Rais amekuwa akipambana sana kuhakikisha miradi inakamilika hivyo lazima tumuunge mkono Rais wetu kwa jitihada anazo zifanya.

" Rais wetu ni  mchapakazi , anafanya kazi kweli miradi anaisimamia kwa fedha zetu za ndani, na hizi fedha ni  kodi zetu sisi wenyewe , kwahiyo tukiwa tunakusanya mapema na kulipa kwa wakati tunahakika nchi hii itapiga hatua" Amesema DAS

Aidha amechukua nafasi ya kuwaaga wananchi Wa Ilala baada ya kupata uteuzi Wa kuwa Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya  Morogoro huku akiwapongeza Wananchi Wa Ilala kwa kuishi nao vizuri na ushirikiano waliompa huku akisema hatawatupa na waendelee kumuunga mkono Rais Dkt John Magufuli pamoja na Mkuu Wa Wilaya Ilala
Mh Sophia Mjema.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.