DC Mjema awashukia wakwepa Ushuru Soko la Buguruni.
.
MKUU wa Wilaya Ilala Mh Sophia Mjema, amewataka wafanya Biashara wa Soko la Buguruni waliohama katika vizimba na kufanya Biashara nje ya soko kwa kigezo cha kuwa na Kitambulisho cha Ujasiriamali warudi Mara moja.
Agizo hilo amelitoa Leo Oktoba 30/2019 katika ziara yale kufuatia malalamiko ya baadhi ya wafanya Biashara wa Soko hilo. Aidha katika Kuona suala hilo linafanyiwa kazi, amemuagiza Afisa Masoko, Ndugu Ally Baruani , kufanya kikao na wafanya Biashara hao Mara baada ya ziara kumalizika ili kuwarudisha ndani ya Soko kwani kitendo hicho kinainyima Manispaa mapato. Pia amesema wale watakao kaidi watachukuliwa hatua za kisheria.
DC amesema kuwa Soko hilo lipo kwa ajili ya manufaa ya wafanyabiashara wote na sio kwa watu wachache.
" Kwa hili sitowasamehe, mnawaumiza wenzenu, kwaninni mkwepe ushuru wakati wenzenu wanipa, nataka mrudu haraka na wasio taka tunawachukulia hatua, " Amesema Mjema.
Aidha amesema kutumia vitambulisho vya Mjasiriamali ni kosa kubwa kwani mfanya Biashara yeyote anayefanya sokoni kwa kupangiwa kizimba anapaswa kulipa ushuru kwa mujibu wa Sheria za Soko na utaratibu, kwani kutofanya hivyo kunaikosesha seeikali mapato .
Amesema anatambua wote wafanya Biashara lakini kila mfanya Biashara anatambulika kwa mujibu wa Sheria na kanuni , hivyo wanaostahili vitambulisho vya Mjasiriamali na mlipa ushuru sifa zao zinatofautiana.
Mbali na wakwepa ushuru amewataka madalali wa Biashara waache kuwakandamiza wafanyabiashara badala yake watumie mikataba katika makabidhiano yao ya kibiashara.
Aidha amesema wale madalali watakaoonekana wanakiuka Sheria wataondolewa katika Soko hilo .
Kwa upande wa Mkurugenzi Manispaa Ilala Mh Jumanne Shauri, ameshauri kuwepo kwa mikataba maalumu ya kisheria kati ya mfanya Biashara na Dalali ili kila mmoja kuweza kunufaika.
Post a Comment