DC Mjema atembelea mradi wa Maji Majohe wenye thamani ya Shilingi Milioni 200 na kuitaka kamati ya Maji kuwa waaminifu katika kuwanufaisha Wananchi.
MKUU wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema ametembelea mradi wa ujenzi wa mradi wa maji mtaa wa Kichangani Kata ya Majohe wenye thamani ya sh milioni 229,667,088 ambao utakamilika Oktoba 30 mwaka huu.
Ujenzi wa mradi huo unaojengwa na Sk Building and Civil Engineering ambao mpaka sasa umekamilika kwa asilimia 95 na utakapokamilika utawasaidia zaidi ya wananchi 150,000 wa Kata hiyo.
Akizungumza Jana jijini Dar es Salaam, wakati wa ukaguzi wa mradi huo, Sophia alisema ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa mradi huo ambao utawasaidia wananchi wa Kata hiyo kupata maji ya uhakika.
Alisema ameamua kutembelea mradi huo ili kuona ujenzi unaendeleaje na kama kuna changamoto basi aweze kuona ni namna gani wanazitatua.
"Mimi jukumu langu kuja kuona maendeleo yanayofanyika ili kama kuna changamoto yoyote tuone tunafanya nini lakini nimefurahishwa sana na kazi na natumaini wananchi watapata hitajilao na natumaini mradi huu utakamilika kweli Oktoba 30 mwaka huu "alisema
Pia aliwataka viongozi wa Kata hiyo pindi mradi huo utakapo kamilika kuhakikisha wanasimamia vizuri mradi huo ili wananchi waweze kupata huduma ipasayo.
"Serikali imesikia kilio cha wananchi na kujenga mradi huu sasa sitaki kusikia mradi huu aujaendelezwa na badala yake nataka watu wapate maji"alisema
Kaimu Mhandisi wa Maji, Kheri Sultani alisema kukamilika kwa mradi huo kutakwenda kumaliza changamoto ya uhaba wa maji katika eneo hilo.
"Wakina mama wengi walikuwa wanapata shida ya maji hivyo serikali kupitia mradi huu utakwenda kumtua ndoo kichwani mama "alisema
Mlezi wa Kata hiyo, Zena Mwiko alisema mradi huo utawasaidia wananchi wa Kata hiyo kwani changamoto ya maji kwao ilikua ndiyo tatizo kubwa.
Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Wilaya ametembelea Daraja la Viwenge ambalo limegharimu kiasi cha sh milioni 60 na kuagiza Tarura kujitaidi kutatua changamoto ndogondogo ambazo zimebaki ili pindi mvua zinapokuja zisiathiri daraja hilo.
"Daraja ili nimeona mmejenga vizuri lakini naomba muweke ukingo pembezoni kwani mvua zinaponyesha zitaweza kupukuchua ardhi ya pembeni na daraja kubaki Katikati "alisema
Ofisa wa Tarura, Sauda Bwile alisema amelipokea ushauri wa Mkuu wa Wilaya na atahakikisha analifikisha ofisini ili kuanza utekelezaji.
Zuhura Abdallah ambaye ni mwananchi wa Viwege alisema anishukuru serikali kwa kuwajengea daraja ilo ambalo zamani eneo hilo wakati wa mvua lilikuwa alipitiki.
"Daraja ili linatusaidia kwakweli kwani hapo awali mvua zikinyesha watoto awaendi shule lakini pia hata sisi wananchi tulikua tunashindwa kufanya shughuli za maendeleo"alisema
Mkuu wa Wilaya Sophia ambaye yupo kwenye ziara ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi sambamba na kukagua miradi ya kimaendeleo inayoendelea katika wilaya hiyo.
Post a Comment