Meya Manispaa Ilala afunguka juu ya huduma za uzalishaji Hospitali ya Mnyamani zilivyoimarika.
MEYA wa Manispaa ya Ilala na Diwani Kata ya Vingunguti, Mh Omary Kumbilamoto, amesema kuanzia tarehe 1 Novemba mwaka 2019, huduma za upasuaji wa Wakina mama Wajawazito zitatolewa bure. .
Ameyasema hayo mbele ya Waandishi wa Habari, wakati akijibu baadhi ya kero za Wananchi kata ya Mnyamani katika ziara ya Mh Sophia Mjema Mkuu wa Wilaya Ilala kutembelea kata hiyo.
Amesema tayari vifaa vyote vimeshafika vya upasuaji , ambapo milioni 100 zimeshaingizwa katika hospitali hiyo kwa ajili ya upauaji wa mabati katika vyumba 14.
" Nipende kumjibu Mzee wangu, sisi sio kams tumelala tunakula viyoyozi bali tunapambana kuwaletea Maendeleo nyinyi Wananchi, lakini nitoe rai kwa watendaji katika kutatua kero sio kukaa ofisini inabidi tutoke nje ya Ofisi kuwafuata Wananchi kama anavyofanya mama Mh Sophia Mjema Mungu akubariki sana unafanya kazi sana umekuwa chachu ya Maendeleo ya ilala" Amesema Kumbilamoto.
Katika kujibia kero ya mradi wa PMM, amesema mradi huo Wananchi wahusahau badala yake watafute mpango mwengine wa kumpa tenda mtu mwengine, ikiwezekana watu warudishiwe leseni zao za Makazi.
" Huyu mama wa PMM amechemka kufuatia agizo la Waziri Lukuvi hivyo watu wa benki wakarudi nyuma, lakini kitu pekee kitakachotukombo ni mradi wa PMM Phrase 3 ambao uliwekewa Bilioni 115 na Serikali ukatengeneza bara bara za Kiwalani na Gongolamboto, kwahiyo Serikali imeingiza Bilioni 1 na milioni 500 " Amezidi kufafanua Kumbilamoto.
Kuhusu Ofisi ya kata, amemtaka Diwani wa Kata hiyo kutembea kifua mbele kwani wameshapata nyumba na wapo katika mchakato wa kumuingizia Diwani pesa kwa ajili ya ukarabati.
Pia amesema kutokuwepo kwa shule ya Msingi na Sekondari katika kata hiyo kumetokana na Wananchi wenyewe baada ya maeneo mengi kutokuwa na leseni za makazi, hivyo zitavyotoka watajenga haraka shule ili kukamilisha mpango wa Rais Dkt John Magufuli wa Elimu bure.
Post a Comment