Header Ads

DC Mjema aridhishwa na kasi ya Ujenzi wa Mradi wa Nyumba za Magereza Ukonga















MKUU Wa Wilaya ya Ilala, Mh Sophia Mjema, amerishishwa na kasi ya ujenzi unaoendelea Wa Ghorofa 12 Wa Nyumba za Maofisa Gereza la  Ukonga. .

Hayo ameyasema leo  kwenye muendelezo wake Wa ziara alioufanya leo  Oktoba 1/2019 Kata ya Kariakoo na Mchikichini. Akizungumza na Waandishi Wa Habari, amesema hatua iliyofikia ni  nzuri hivyo amelipongeza Jeshi la  JKT kwa kazi nzuri waliyoifanya.

Aidha amesema kwamba  kasi waliyonayo ndio kasi anayoitaka Mh Rais Dkt John Magufuli.

" Tunawapongeza kwa kazi kubwa, Mh  Rais kawapa kazi hii akiwa na mategemeo makubwa kwenu hamjamuangusha mmefanya kazi huu ndio uzalendo, kwahiyo endeleeni kumuunga mkono kwa kupiga kazi ili mradi huu uweze kukabidhiwa mapema kama mlivyopanga" Amesema DC Mjema.

Mbali na kukagua ujenzi huo, pia amepata nafasi ya kutembelea Wafungwa waliopo katika adhabu ya kunyongwa huku akiwataka waishi kwa matumaini na waamini katika maisha chochote kinawezekana.

 " Natambua sana mmenieleza changamoto zenu lakini kikubwa ninachokiona ni kukosa uhuru, mtafanya vyote lakini kama huna uhuru maisha yatakua magumu sana, niwaombe ombeni sana kwa mungu na muwe na matumaini huku mkimuombea Rais wetu Afya nzuri katika majukumu yake" Ameomgeza DC Mjema.

Naye Mhandisi wa  Mradi huo, Luteni Samwel Machemba, amesema mradi huo hadi kufikia Oktoba 30 mwaka huu watakuwa wameshaukabidhi.

Amesema mradi huo utachukua jumla ya Watu 172 ambapo miongoni Nyumba hizo zenye ghorofa 12, Askari watakuwa na Nyumba 136 na Nyumba 36 kwa ajili ya maafisa Wa Magereza. Aidha amesema kukamilika kwa mradi huo utagharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 3.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.