DC Mjema aridhishwa na kasi ya ujenzi wa Daraja Jipya la Salender.
MKUU wa Wilaya Ilala Mh Sophia Mjema , ameridhishwa na kasi ya Ujenzi wa Daraja Jipya la Salender wakati alipofanya ziara yake ya kukagua Maendeleo ya mradi huo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Oktoba 9/2019, amesema kasi ya Ujenzi huo unaridhisha hivyo waongeze Nguvu ili ikifika muda waluopangiwa wawe wameukabidhi miradi huo kwa Serikali. .
Aidha amefurahishwa na kuwepo kwa wimbi kubwa la Watanzania waliopata ajira katika mradi huo..
Amesema mradi huo utakapokamilika utawasaidia Watanzania kupata ujuzi zaidi juu ya Ujenzi wa madaraja makubwa kwani wasimamizi wa mradi huo wamekuwa na utaratibu wa kuwafundisha ujuzi na jinsi ya kujenga.
" Tunawapongeza sana, kwanza wapo mbele kwa asilimia 2% tangia wakabidhiwe mradi huo , tunawaomba wafanye kazi kwa bidii na kwa haraka ili ule muda uliowekwa ukifikia wawe wamekabidhi mradi huo " Amesema Mjema.
Katika hatua nyingine, amechukua nafasi ya kumpongeza Mh Rais Dkt John Magufuli kwa kutekeleza miradi mikubwa hapa nchini, huku akisema miradi hiyo inatakiwa kuongezeka ili Watanzania waweze kupata ajira.
Pia amewatahadharisha Wavuvi pamoja na wafanya biashara wasikatize eneo la mradi kwani ni kunaweza kusababisha hatari kubwa kutokana na Ujenzi huo kutokamilika na vyuma vinaanguka.
Naye Meneja Usalama, Mazingira na Afya, Ndugu Acme Mutabilwa, amesema Daraja hilo linatarajia kukamilika Oktoba 10 mwaka 2021.
Amesema mpaka sasa wamefikia 16% ambapo mradi huo utakuwa na Kilomita za Mraba ( KM 1.7), na mradi huo unaanzia Ofisi ya Mkemia wa Serikali hadi Agakhan Hospitali ambapo patakuwa na makutano ya bara bara . .
" Mradi unaendelea vizuri, kuna 92% ya Watanzania wanaofanya kazi sawa na watu 430 hadi 500 na wafanyakazi 28 kutoka nje , tulikabidhiwa mradi Oktoba 152018 na tutamaliza Oktoba 10 /2021 au chini ya hapo kulingana na ushirikiano mzuri kutoka kwa TANROAD" Amesema Amesema Mutabilwa.
Post a Comment