Header Ads

DC Mjema apiga marufuku Malori kutembea mchana kati kati ya Mji.

.






MKUU Wa Wilaya ya Ilala, Mh: Sophia Mjema, amepiga marufuku Malori kutembea mchana huku akidai upo  utaratibu uliowekwa.

Akizungumza na Wananchi Kata ya Kariakoo Kaskazini na Kata ya Mchikichini Leo Oktoba 1/2019,amesema kuwa Malori yote yanatakiwa kuanza safari kuanzia saa  12:00 Jioni hadi  saa  12:00 Asubuhi zaidi ya hapo hatua Kali za kisheria zitachukuliwa.

 Amemuagiza OCD Ilala kuhakikisha wale wote  wanaoegesha Malori na kuendesha mchana kunyang'anywa Leseni zao na kupigwa faini kwani wanahatarisha Usalama Wa Wananchi pamoja na msongamano Wa foleni.

" Namuagiza OCD ukikuta Malori yanaendeshwa mchana katika Wilaya yangu au yameegeshwa yakamateni na wachukulieni hatua, unajua pembezoni Mwa bara bara kuna watu wanafanya Biashara sasa haya Malori kuna muda yanaanguka hovyo kwahiyo anzeni sasa ili kero hiyo tuimalize" Amesema DC.

Pia amesema kero  zote ifikapo Desemba mwaka huu ziwe zimetatuliwa.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.