Header Ads

Bajaji Bonyokwa wafurahishwa na maamuzi ya DC Ilala.





KIKUNDI cha Bajaji kinachojulikana kwa jina la  KIWABASE , Kata ya Segerea Mtaa Wa Bombani, wamefurahishwa na kitendo cha Mkuu Wa Wilaya Ilala, Mh Sophia Mjema,  kutoa agizo Bajaji hizo kufanya kazi  za kupakia Abiria baada ya SUMATRA kuwazuia kufanya kazi.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti mbele ya vyombo vya Habari leo  Septemba 27/2019 , wamemshukuru DC Mjema kwa uamuzi wake huku wakimuomba kulitatua suala hilo  ili waweze kupata ridhiki.

Aidha, Makamu Mwenyekiti Wa Umoja huo, Ndugu Yunus Abdi, amesema umoja huo unajumla ya wanachama 100 ambapo wamefanya kazi  zaidi ya miaka 10 hawajafukuzwa.

 Amesema kukaa kwao bila kazi kunapelekea ugumu Wa maisha na kushindwa kurudisha pesa kwa matajiri wao.

 Amesema kuwa baada ya kunyang'anywa vibali ikiwamo SUMATRA,Bima pamoja na Leseni. " Fanyeni kazi lakini Jumatatu njooni Ofisini kwangu tuweke mambo sawa ili mtafute ridhiki zenu" Amesema DC Mjema.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.