Header Ads

Mkurugenzi Manispaa Morogoro awakaria kooni watoa rushwa kuelekea uchaguzi Serikali za Mitaa.







 MKURUGENZI Wa Manispaa ya Morogoro Mjini, Mh Sheila Lukuba, amesema hawatawafumbia macho viongozi watoa rushwa kuelekea Uchaguzi Serikali za Mitaa.

 Hayo ameyasema leo Oktoba 8/2019   wakati Wa Ziara ya kukagua Vituo vya kujiandikisha wapiga kura katika Halmashauri hiyo.


  Akizungumza  na Waandishi Wa Habari, amesema wamejipanga na tayari Takukuru wapo mitaani kwa ajili ya kuangalia vitendo vya rushwa na watakaobainika hatua Kali za Sheria zitachukuliwa


" Tumejipanga vizuri, tunataka Viongozi watakaochaguliwa wawe waadilifu na wapite kwa matakwa ya Wananchi wao na sio kwa kutumia Nguvu ya pesa, tukiwabaini wala rushwa na watoa rushwa wote tutawachukulia hatua" Amesema Sheila.


Hata hivyo, amewaomba Wananchi wajitokeze kwa wingi kujiandikisha ili kuweza kuwapata Viongozi watakao tatua kero zao.

 Amesema Rais Mh Dkt John Magufuli anataka Viongozi wachapa kazi ili kuleta Maendeleo.

Katika hatua nyengine amewataka watumishi nao kujiandikisha kupiga kura kwani baadhi yao wanajisahau na ni haki yao ya Msingi na kikatiba.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.