Mkurugenzi Manispaa Morogoro awapa wiki Moja wafanyabiashara Hoteli kubwa kulipa madeni kabla hawajafikishwa Mahakamani.
MKURUGENZI wa Manispaa ya Morogoro Mh Sheila Edward Lukuba, amewapa ametoa wiki moja kwa Hoteli kubwa zenye madeni ya kodi kulipa kabla hawajafikishwa Mahakamani.
Amezungumza hayo Leo Oktoba 30/ 2019, katika ziara ya kukagua leseni kwa wafanya Biashara katika Manispaa hiyo.
Amesema zipo Hoteli kubwa tangia mwaka 2018 hawajalipa kodi, hivyo kuanzia tarehe 1 Novemba mwaka huu 2019 waanze kulipa madeni hayo kabla ya kuchukuliwa hatua.
" Kila mtu anahitaji mapato hivyo wao wanafaida na sisi tunataka faida, kwani tuna miradi mbali mbali tunahitaji kuifanya ikiwamo miradi ya shule, Vyoo, Maabara pamoja na Mifuko ya Mikopo ya kuwawezesha kiuchumi, Vijana, Wakina mama pamoja na Walemavu" Amesema Sheila.
Amesema wakikaidi kulipa madeni hayo watawafikisha Mahakamani na kama itashindikana watawafikisha kwa Waziri wa TAMISEMI, Mh Suleiman Jaffo, kwa ajili ya msaada zaidi.

Post a Comment