Kamati za shule zinatakiwa ziwe wabunifu kuleta Maendeleo ya Elimu: DC Mjema.
Hayo ameyasema Leo Oktoba 21 mwaka 2019, katika ziara yake Kata ya Segerea ya kuzungumza na Wananchi katika utatuzi wa kero zao.
Amezungumza hayo, mara baada ya kupokea kero ya Mwananchi kuhusu malalamiko ya kutokuwepo kwa uzio katika Shule.
" Wananchi tutambue Serikali ya awamu ya tano, chini ya Rais Dkt John Magufuli imeweka Elimu bure kuanzia Shule za Msingi na Sekondari, hivyo kuwepo kwa kamati za shule ni Kuona mnakuwa wabunifu katika kutatua kero nyengine zinazojitokeza katika kuleta Maendeleo ya shule zetu" Amesema Mjema.
Naye Kaimu Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Ilala , Bi Asha Mapunda, amesema mpango wao katika Elimu ni kutoa Elimu bure na sio ujenzi wa uzio, hivyo kama kuna ulazima kamati zikae zione namna ya kupanga mipango ili kusaidiana katika kutatua kero hiyo
Post a Comment