Header Ads

T.A.G USHARIKA MWEMBESONGO WAKABIDHI MADAWATI 100 SHULE YA MSINGI MAFISA "A"


KANISA la Tanzania Assemblies of God (T.A.G) , Bethel Revival Temple, Mtaa wa Mwembesongo Manispaa ya Morogoro chini ya Mchungaji wake, Dkt. Barnabas Mtokambali  wamekabidhi jumla ya Madawati 100  Shule ya Msingi Mafisa A Kata ya Mwembesongo.

Madawati hayo yamekabidhiwa Novemba 03/2023 yakipokelewa na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro , Gabriel Paul pamoja na Uongozi wa Kata ya Mwembesongo wakiongozwa na Diwani wa Kata hiyo Mhe. Ally Kalungwana.

Akizungumza wakati wa kukabidhi Madawati hayo, Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (T.A.G) , Bethel Revival Temple lililopo Mtaa wa Mwembesongo Manispaa ya Morogoro , Dkt. Barnabas Mtokambali , amesema msaada huo ameutoa kutokana na kilio cha wanafunzi hao alipokuwa mgeni rasmi katiia moja ya Mahafali ya Shule hiyo.

Dkt. Mtokambali, amesema msaada huo utaondosha kero ya wanafunzi darasani  kwani awali walikuwa na changamoto ya Madawati 75 na T.A.G imeona waongeze Madawati na kufikia 100.

"Leo  tumetimiza kiu ya changamoto ya watoto wetu, tulipokuja hapa walisema upungufu ni Madawati 75 l;akini nimekaa na wazee wangu wa Kanisa wakasema tuwape 100 ili tumalize changamoto yao na leo tumetimza ahadi yetu "Amesema Dkt. Mtokambali.

Kwa upande wa Kaimu Mkurugenzi Manispaa ya Morogoro, Gabriel Paul, ameshukuru Kanisla la T.A.G kwa  msaada wao wa Madawati 100 huku  akisema kuwa msaada huo utaondosha kero ya wanafunzi darasani na hakuna mwanafunzi ambaye atakosa sehemu ya kukaa.

"Tunawashukuru wadau wetu, haya madawati watoto wetu wote watakaa kwenye nafasi zao, lakini hata waalimu utawapa nafasi nzurri ya kufundisha na wanafunzi wakaelewa vizurri darasani, milango ipo wazi Manispaa karibuni wadau kwa maoni, ushauri na misaada sisi kama Serikali tutaendelea kutoa ushirikiano" Amesema Gabriel.

Naye Diwani wa Kata ya Mwembesongo, Mhe. Ally Kalungwana, T.A.G  wamekuwa msaada kwa Kata hiyo kwani wamekuwa wakiwa karibu na changamoto za wana Mwembesongo.

“Niseme kutoka moyoni nimepata faraja kubwa kwa ndugu zetu kutukumbuka,wamekuwa msaada mkubwa sio kwenye madawati , wamekuwa wakitusaidia a katika Nyanja mbalimbali zikiwemo za Elimu, Afya, Mazingira na huduma nyengine za kijamii. ,na hili pia la kutupa madawati ni  tukio jema la faraja” Amesema Kalungwana.




No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.