WANANCHI wa Kata ya Mafiga Manispaa ya Morogoro, wametakiwa kuwa na imani na Serikali ya Chama cha Mapinduzi ( CCM) katika utekelezaji wa Ilani yake kwa Wananchi hasa katika sekta mbalimbali katika kuwaletea wananchi maendeleo.
Hayo yamezungumzwa na Diwani wa Kata ya Mafiga, Mhe. Thomas Butabile, katika muendelezo wake wa ziara ya kusikiliza kero za wananchi na kurejesha yale ambayo ameyafanya katika kipindi cha miaka 3 ya Uongozi wake katika Mtaa wa Kidondolo A.
Kuhusu suala la changamoto ya Maji, Mhe. Butabile, amesema Sekta ya maji ni moja kati sera ya Chama cha Mapinduzi na kuongeza kuwa Chama hicho kitaendelea kuisimamia Serikali katika kuhakikisha kuwa sera za Chama hicho zinatekelezwa ipasavyo kwa Wananchi ikiwemo ile ya maji hasa katika maeneo ambayo huduma hiyo imekuwa haipatikani.
“Chama cha Mapinduzi ndio jawabu ya majibu ya matatizo ya Watanzania na sii kukimbilia chama kingine ambapo ni sawa na kutokuwa na mwelekeo na majawabu ya majibu yenu hayawezi kupatikana”, Amesema Mhe. Butabile.
Butabile, amesema Wana Mafiga wanajivunia sana uwekezaji wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwani katika kipindi cha miaka yake 3 tangia aingie Mdarakani tayari Kata ya Mafiga imekuwa Kata ya mfano katika kukuza sekta ya elimu kwa ongezeko la ufaulu Shule za Msingi na Sekondari pamoja na ujenzi wa madarasa.
Aidha, Butabile, amewataka wananchi wa Mafiga kuwa na imani na Chama cha Mapinduzi kwani kimewatoa mbali tangu uhuru na ndio chama pekee inachoweza kutatua matatizo ya Watanzania pamoja na kero za mbalimabali walizo nazo.
Mwisho Butabile, amewaomba wana CCM Kata ya Mafiga kutokana na kazi kubwa anazozifanya Rais Samia, wanachama cha Mapinduzi wasisite kuzungumzia maendeleo kwa kipindi hiki cha sasa.
Miongoni mwa mafanikio ambayo yamepatikana katika kipindi cha miaka 3 ya Mhe. Butabile ni ujenzi wa Madarasa 3 nguvu za Wananchi Shule za Msingi Misufini B , Shule ya Msingi Mafiga B, ujenzi wa Ofisi ya Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Mafiga B, Ujenzi wa Ofisi ya Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Misufini B, Ujenzi wa Uzio Shule ya Msingi Misufini A, Ufaulu wa asilimia 100 kidato cha Sita Shule ya Sekondari Mafiga kwa miaka 3 mfululizo bila kuwa na sifuri, uboreshaji miundombinu ya barabara, vikao vya kusikiliza kero awamu zote tatu, kushinda tuzo za usafi kwa upande wa Mitaa n.k.
Ziara ya Mhe. Butabile itaendelea tena Novemba 03/2023 katika Mtaa wa Kidondolo B akiwa na Timu ya wataalamu kutoka Maadili, Jeshi la Zima Moto, TAKUKURU, TARURA pamoja na huduma za Lishe.
Post a Comment