BUTABILE AWAPA TANO MORUWASA
DIWANI wa Kata ya Mafiga Manispaa ya Morogoro Mh. Thomas Butabile, ameipongeza Idara ya Maji Mkoa wa Morogoro , MORUWASA chini ya Mkurugenzi wake, Eng. Tamimu Katakweba, kwa utekelezaji wa miradi ya maji katika Kata yake.
Hayo ameyasema katika muendelezo wa ziara yake ya kusikiliza , kutatua kero za wananchi na kutoa mirejesho kwa kile ambacho Serikali imefanya na ambacho amekifanya katika kipindi cha miaka 3 yake tangia aingie madarakanni mwaka 2020 akiwa Mtaa wa CCM.
Butabile,amesema MORUWASA wamekuwa wasikivu kusikiliza kero za wananchi katika huduma ya maji, kwani katika ziara zake za Mitaa likutana na kadhia ya maji lakini baada y akuunda kamati na kufika Ofisi za MORUWASA tayari MORUWASA wapo kazini kuhakikisha changamoto za maji Kata ya Mafiga zinaondoka.
Hatua walizofikia MORUWASA ni kufunga mabomba ya Maji pamoja na kuunganisha Mita ili wananchi waendelee kupata huduma za maji.
Akizungumza kwa njia ya simu, Mkurugenzi wa MORUWASA, Eng. Tamimu Katakweba, amempongeza Diwani wa Mafiga kwa kutambua changamoto na amesema wananchi wasisite kutoa taarifa kwani MORUWASA ipo kwa ajili ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za Maji.
Post a Comment