WANANCHI MAFIGA WAKUNWA NA UTENDAJI KAZI WA DIWANI BUTABILE.
WANANCHI wa Kata ya Mafiga Manispaa ya Morogoro , wampongeza Diwani wa Kata hiyo, Mh. Thomas Butabile kwa kazi kubwa anayoifanya kwa kushirikiana na Uongozi wake wa Kata.
Pongezi hizo zimetolewa Novemba 10/2023 na wananchi katika mwendelezo wa ziara ya Diwani huyo ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi pamoja na kutoa mirejesho ya Serikali ilichofanya katika Kata hiyo pamoja na kazi zake tangia aingie madarakani mwaka 2020 kwenye Mtaa wa Mafiga B.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti tofauti, Wananchi hao wameeleza kuwa katika kipindi Cha miaka iliyopita Mafiga haikuwa na maendeleo makubwa kama haya ambayo inayo sasa kama vile Stendiya Daladala, miundombinu bora, elimu bora na viwango vya ufaulu wa juu kwa wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari.
Wananchi hao kupitia yale ambayo Diwani wao anayowafanyia wamesema wataendelea kumuunga mkono bega kwa bega ili atimize ahadi zake ili kuendelea kuwaletea wananchi maendeleo.
Naye, Mhe Butabile , ameeleza kuwa anaendeleza pale anapoishia kwa kuleta maendeleo na fkira chanya Kwa Wana Mafiga.
" Mafisa Sasa hivi inakimbia na haitembei kwa kuwa tayari tunayo bandari kavu katika soko la zamani manzese ambapo malori yote yanashusha mizigo katika soko lile na imepelekea baadhi ya wanamafiga kupata ajira pale na kujihusisha na ujasiriamali mdogo mdogo, lakini hata seketa ya elimu tumepiga hataua sana leo ufaulu umeongezeka sana ,Sekondari Kidato cha Sita hakuna sifuri wote wamefaulu kujiunga na Vyuo Vikuu haya ni maendeleo makubwa sana "Amesema Mhe. Butabile.
Vilevile, Mhe. Butabile amewashukru viongozi wote wa Kata hiyo na wananchi kwa ujumla kwa kumuunga mkono katika kazi anazofanya na amewaomba waendelee kumpatia ushirikiano.
Mwisho amekipongeza Chama chake Chama Cha Mapinduzi CCM kwa ushirikiano mkubwa wanaompatia katika kutekeleza vyema Ilani ya CCM.
Ziara ya Mhe. Butabile itaendelea tena katika Mtaa wa Zahanati Novemba 9/2023.
Post a Comment