DIWANI BUTABILE ALIVALIA NJUGA SUALA LA CHANGAMOTO YA MAJI MAFIGA
DIWANI wa Kata ya Mafiga Mhe. Thomas Butabile, amewahahkikishia wananchi wa Kata ya Mafiga kuwa lengo lake kwa sasa ni kuhakikisha suala la maji linapatiwa ufumbuzi.
Hayo ameyasema Novemba 03/2023 katika Mkutano wa Wananchi wa Kusikiliza kero na kutoa mrejesho kwa kile alichokifanya katika kipindi cha miaka yake 3 ya Uongozi Mtaa wa Kidondolo B.
Butabile, amesema anatammbua changamoto ya Maji katika Kata yake, hivyo amewaomba wahusika wa Mamlaka ya Maji MORUWASA kuhakikisha yale maeneo ambayo yana changamoto ya maji yaangaliwe kwa kina.
Katika kuona hilo linakamilika, Mhe. Butabile, ameunda kamati ya ikiwa na lengo la kufuatilia huduma ya maji pamoja na kwenda kwa Mkurugenzi wa MORUWASA ili kuona namna ya kutatua kero hiyo.
"Changamoto hii sio ya Mtaa wa Kidondolo B pekee , hapa nimeambiwa miezi 2 maji hakuna na bili inaletwa kubwa , tatizo hili sio kwa Mtaa huu ni mitaa mingi inachangamoto hizi, niombe Kamati hii ambayo ina changamoto ya maji hakikisheni maji yanapatikana" Amesema Butabile.
Katika hatua nyengine, Mhe. Butabile, ameagiza Taasisi zote za Umma ambazo zina huduma ya Visma vya maji ikiwemo Shule pamoja na Stendi ya Daladala Mafiga zihakikishe oia huduma hiyo ya maji zinahamishiwa kwa wananchi huku wakisubiria changamoto ya maji kupatiwa ufumbuzi .
Kwa upande wa Afisa Masoko MORUWASA , ambaye jina lake limehifadhiwa amekiri kuwepo kwa tatizo la maji huku akiwataka Wananchi kutoa taarifa kwa wakati wanapoona changamoto hiyo.
Amesema MORUWASA wapo kwenye mpango wa wananchi kulipia bili kama wanavyofanya TANESCO ambapo huduma hiyo tayari ipo katika Hospitali ya Rufaa ya Morogoro ambapo wanalipa maji ndipo wanatumia huduma ya maji ili kuepusha usumbufu.
Ziara ya Mhe. Butabile itaendelea tena siku ya Jumatatu ya tarehe 06/2023 kwenye Mtaa wa Misufini akiendelea kuhakikisha kero za Kata yake zinapatiwa ufumbuzi.
Post a Comment