BUTABILE AWAPONGEZA NIDA KWA KUWAJIBU WANANCHI KWA WAKATI.
DIWANI wa Kata ya Mafiga Manispaa ya Morogoro, Mhe. Thomas Butabile, ameipongeza Ofisi ya NIDA kwa kusikiliza kero za wananchi za kusogezewa huduma ya vitambulisho vya uraia katika Kata yao.
Pongezi hizo amezitoa Novemba 15/2023 katika Mtaa wa Kambaya wakati wa mwendelezo wa ziara yake ya kusikiliza,kutatua kero za Wananchi na kutoa mrejesho kwa yale aliyoyatekeleza na anaendelea kutekeleza.
Butabile amesema kuwa amefurahishwa Sana na jitihada za NIDA kwa kuwapatia vitambulisho kwenye Kata ya Mafiga kwa kuwa ilikuwa ni changamoto kubwa na wananchi walikuwa wanalalamikia sana utendaji kazi wao.
" Nawakaribisha Sana kata ya Mafiga tuendelee kufanya kazi kwa Kushirikiana, najua NIDA mna kazi kubwa katika Mkoa wetu wa Morogoro lakini hiki mlichokifanya kwetu ni faraja sana kunapokuwa na tatizo tuwasiliane, mdogo wangu James Afisa NIDA hongera sana kusikia Vilio vya wana Morogoro "Amesema Butabile.
Naye Afisa mtendaji wa kata hiyo Bi, Amina Said Mhina amekili kupokea vitambulisho hivyo katika ofisi yake na kusema amepokea vitambulisho visivyopungua 5,700 na bado vitaletwa vingine.
Bi, Amina amewaamini wananchi kuwa tayari vitambulisho vipo ofisini kwake kwa kumkabidhi Mh Butabile kitambulisho chake.
Aidha, wananchi wameridhishwa na utendaji kazi wa viongozi hao na kuwaomba wazidi kuwa na ushirikiano ili kuhakikisha wanaleta mabadiliko chanya ndani ya kata hiyo.
Post a Comment