WANANCHI MAFIGA WATAKIWA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA SERIKALI.
WANANCHI wa Kata ya Mafiga Manispaa ya Morogoro wametakiwa kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kufanya kazi kwa bidii ili dhamira ya dhati ya Serikali inayolenga kuleta maendeleo kwa kila mtanzania iweze kutimizwa.
Rai hiyo imetolewa Novemba 09 /2023 na Diwani wa Kata ya Mafiga, Mhe. Thomas Butabile, akiwa katika ziara ya kikazi ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi pamoja na kutoa mirejesho ya kile Serikali ilichokifanya katika Kata yake akiwa Mtaa wa Polisi ikiwa ni muendelezo wa ziara yake.
"Kuna baadhi ya wananchi wanalalamika kuwa serikali haifai ila serikali inafaa ndiyo maana wanashuka chini kusikiliza kero zao , hata katika vikao vayngu hivi nilivyo vianza mmeona namna ninavyo washirikisha wataalamu kutoka Taasisi mbalimbali za Umma na mmeona namna wanavyosikiliza na kutolea ufafanuzi wa kero husika na wamekuwa pia wakitupa elimu zaidi juu ya Taasisi zao zinavyofikika na kutoa huduma " Amesema Mhe. Butabile.
Aidha, Butabile amewataka Watendaji wa Mitaa kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika kusimamia miradi ya maendeleo inayolekezwa katika Mitaa yao.
Butabile,amesema Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imekuwa na mchango mkubwa hususani katika Kata ya Mafiga kwani Mafiga imepokea fedha nyingi za miradi ya Maendeleo kutoka Serikali Kuu ikiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasa, katika shule, madawati , maabara shule ya Sekondari pamoja na miradi ambayo imelekezwa katika huduma za afya.
Hata hivyo, Mhe. Butabile, amewataka Wananchi wa Mafiga waendelee kumuunga mkono Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini, Mhe. Dkt. Abdulaaziz Abood kwani ana mchango mkubwa katika Kata hiyo hususani katika sekta ya elimu kwani amechangia kuingizwa kwa Umeme shuleni, madawati na kutoa mifuko 100 ya saruji , Compyuta na Projecta Shule ya Sekondari Mafiga.
Post a Comment