Header Ads

KISHINDO CHA MIAKA 3 YA DIWANI KATA MWEMBESONGO UTEKELEZAJI MIRADI YA MAENDELEO

MIAKA  3  sasa tangu  Diwani wa Kata ya Mwembesongo Mhe. Ally Kalungwana kuapishwa na kuingia madarakani baada ya uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

Mara baada ya Kuapishwa, Mhe. Kalungwana kwa kuashirikiana na Diwani Viti Maalum , Mhe. Hadija Kombo Kibati na BMK yake , alianza kutekeleza na  kusimamia  miradi mbalimbali ya Kata kwa kushirikiana na Wananchi wake pamoja na kuongozwa na Chama chake kilichompa Dola Chama Cha Mapinduzi CCM .

Kwa kipindi cha Miaka 3, Mhe. Kalungwana  ameendelea na utekelezaji  wa shughuli za Serikali na usimamiaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambapo katika miaka 3 aliyopo madarakani zipo fedha mbalimbali zimetumika kwenye miradi ikiwemo fedha zake binafsi,  fedha za wahisani na wadau  na fedha kutoka Serikali Kuu na fedha kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.

SEKTA YA ELIMU MSINGI 

Katika Idara ya  ya Elimu Msingi, tangia aingie madarakani kwa kushirikiana na Diwani Viti Maalum Mhe. Hadija Kombo Kibati , tayari ujenzi wa madarasa 3 shule ya Msingi Mafisa A kwa nguvu za wananchi na madarasa hayo yapo hatua ya msingi.

Kwa upande wa Shule ya Msingi Mafisa B , tayari amekamilisha ujenzi wa madarasa 3 yenye thamani ya milioni 2,500,000/= fedha kutoka Manispaa na ujenzi upo hatua ya msingi.

Katika shule ya Msingi Msamvu B , tayari ujenzi wa vyumba vya madarasa 3 na matundu ya vyoo 24 vimekamilika ambapo ujenzi huo umetumia milioni 100,000,000/= kupitia mradi wa TEA  na ujenzi umekamilika.

Upande wa Sekondari Mwembesongo, tayari ujenzi wa Jengo la Utawala umekamilika na milioni 100,000,000, zimetumika fedha kutoka Manispaa ya Morogoro.

Ujenzi wa vyumba 3 vya madarasa Shule ya Msingi Mtawala umekamilika na milioni 47,000,000/= zimetumika fedha kutoka Manispaa ya Morogoro pamoja na nguvu za wananchi.

SEKTA YA AFYA

Katika Sekta ya Afya, kwa kipindi cha Miaka 3 ya  Utawala wa Mhe. Kalungwana Kata ya Mwembesongo imeendelea kuimarisha huduma za afya katika Zahanati ya Kata ambapo huduma zimeboreshwa na wananchi wanapata huduma bora ikiwemo dawati maalum la wazee .

Pia, Mhe. Kalungwana ,katika kuona wananchi ambao wana uwezo wa chini wanapata huduma bora, amewakatia wana kaya zaidi ya Kaya 14 bima ya afya ya CHF iliyoboreshwa ili wapate matibabu hayo bure.

Mpango wa TASAF

Kalungwana amesema zaidi ya Milioni 26,604,403 zinaelekezwa kwa ajili ya kaya masikini ambayo inawanufaisha walengwa 248


MIUNDOMBINU YA BARABARA NA MIFEREJI 

katika uboreshaji wa miundombinu ya barabara , Mhe. Kalungwana amesema Manispaa ya Morogoro imetenga Milioni 700 mwaka wa fedha 2023/2024 kwa ajiili ya kununua greda ambalo  litatumika kuboresha barabara za ndani  ya Manispaa ya Morogoro .

Kuhusu mifereji ambayo imekuwa chanzo cha mafuriko mra kwa mara mvua zinavyonyesha , Mhe. Kalungwana amesema tayari mkandarasi amesha saini mkataba na  yupo eneo la kazi kwani mfereji wa Anti- Malaria ni miongoni mwa mifereji ambayo imepitiwa na mradi wa Tactics ambao utekelezaji wake umeshaanza na kupata suluhisho la mafuriko katika Kata hiyo wakati wa mvua.

HUDUMA YA MAJI

Mhe. Kalungwana ,amesema Kata hiyo haina changamoto kubwa sana ya Maji lakini maeneo ambayo kuna changamoto ya maji tayari taarifa ameshazifikisha kwa Mamlaka ya Maji Mkoa wa Morogoro (MORUWASA ).

ANWANI ZA MAKAZI

Kata ya Mwembesongo, ni miongoni mwa Kata 29 ambazo zimenufaika na utekelezaji wa mradi wa Anwani za Makazi ambapo hadi hivi sasa Utekelezaji huo umefikia asilimia 100 ambapo  mradi huo utasaidia Kila Mkazi wa Kata  hiyo kutambuliwa na kurahisisha upatikanaji wa huduma kwani zoezi hilo lilihusisha uwekaji  wa Namba za Nyumba, Majina ya Mtaa na Postikodi ambapo faida kubwa ya anwani za makazi ni kutusaidia kukuza na kuboreshwa kwa huduma za Ulinzi na Usalama ndani ya Jamii, kufanyika na kukuza  kwa biashara Mtandaoni kidigitali na Kusaidia Serikali kufikisha huduma kwa wananchi kirahisi kulingana na Mahitaji ya eneo husika

MRADI WA SOKO.

Mwembesongo imekamilisha ujenzi wa Soko la Kisasa la Mwanzo mgumu ambapo hadi sasa kinachoshangaza ni wafanyabiashara kutokuingia kwenye Soko hilo ambalo limetumia gharama kubwa ya ujenzi .

Mafanikio ya ujumla.

Mhe. Kalungwana amesema yapo mafanikio mbalimbali ambayo katika kipindi cha miaka 3 Kata ya Mwembesongo imeyapata ikiwemo, kupambana na utoro na nidhamu shuleni, ongezeko la madawati 313, ujenzi wa kivuko  (karavati) Mtaa wa Riverside, kupungua kwa wakina mama wanaojifungulia nyumbani, kupisha sheria ndogo, upatikanaji wa vitambulisho NIDA, upatikanaji wa mikopo kwa vikundi 7 vya Vijana, wanawake na watu wenye ulemavu pamoja na uhamasishaji kwa wananchi kujiunga na CHF.

Mikakati 2023-2025

Mhe. Kalungwana, amesema mikakati waliyonayo kwa sasa  ni Uwekaji uzio Zahanati ya Mwembesongo, Ujenzi wa mifereji ya Anti-Malaria, ujenzi wa daraja la Sume, uboreshaji wa miundombinu ya barabara pamoja na ujenzi wa Maabara Shule ya Sekondari Mwembesongo.

Mwisho, Mhe. Kalungwana amesema katika kipindi cha mika 2 iliyobakia ataendelea na Utekelezaji wa Miradi Mbalimbali ya Kimaendeleo ili kukuza Uchumi wa Kata ya Mwembesongo , Kuzalisha ajira na kuongeza Ustawi wa Maisha ya Wananchi wa Mwembesongo  katika kipindi chote cha Utawala wake.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.