BUTABILE AWATAKA VIONGOZI KUZINGATIA MAADILI NA UADILIFU KATIKA KUTOA HUDUMA KWA WANANCHI
VIONGOZI wa Mitaa na wadau mbalimbali watakiwa kuishi kwa maadili na uadilifu ili kujenga nguzo bora yenye kuleta tija katika kukuza na kuchochea maendeleo.
Hayo yamebainishwa na Diwani wa Kata ya Mafiga Mhe. Thomas Butabile, akiendelea na ziara yake katika Mtaa wa Misufini ambapo amesema kufuata maadili siyo matukio bali inapaswa kufanywa kwa maisha ya kila siku .
" Mfano mtu anakunywa hakatazwi lakini unakuta mtu anakunywa mpaka anashindana kuzungusha laundi ukiulizwa unasema nalinda kura au naamasisha wananchi huku ndipo wapo wengi tuache tabia hizo na tujidhibiti na kufanya Kazi ipasavyo kama anavyofanya Rais wetu Dkt. Samia Suluhu hassan ili kuleta maendeleo kwa kasi"Amesema Butabile.
Butabile amewataka wananchi wasisite kutoa taarifa ili kupatiwa haki zao kwa kuwa wao ndiyo wamebeba dhamana ya wananchi.
Naye Afisa wa Maadili mwandamizi Mkoa wa Morogoro,Jackline Msumba, amesema madhara ambayo yanawezwa kuletwa na kiongozi asiyekuwa na maadali ni makubwa hivyo yawapasa kutambua uongozi ni dhamana ya kuhakikisha unatekeleza majukumu uliopatiwa kikamilifu.
Msumba, amewataka Wananchi wa kata ya Mafiga kutoa taarifa mapema endapo kiongozi hatafuata maadili ya Uongozi wake.
"kazi ya Viongozi ni kuhakikisha viongozi wanawatumikia wananchi lakini kwa kufuata kanuni na siyo kuvunja sheria" Amesema Msumba.
Ziara ya Mhe. Butabile imeendelea leo Novemba 07/2023 katika Mtaa wa Polisi akimabatana na wataalamu mbalimbali kutoka Ofisi za Umma pamoja na Ofisi ya Kata.
Post a Comment