WANANCHI MAFIGA WATAKIWA KUTIBIWA KATIKA KITUO CHAO CHA AFYA.
WANANCHI wa Kata ya Mafiga Manispaa ya Morogoro wametakiwa kutibiwa katika Kituo chao cha afya kwani huduma zote zinatolewa hapo kwa masaa 24.
Kauli hiyo ameisema Diwani wa Kata ya Mafiga,Mh. Thomas Butabile, Novemba 20/2023 Mtaa wa Manzese wakati wa mwendelezo wa ziara yake ya kusikiliza,kutatua kero za wananchi na kutoa mrejesho kwa aliyo yafanya ndani ya Kata ya Mafiga.
Aidha,Butabile amefafanua kuwa kitua cha afya mafiga kinaendelea kuwa kikubwa kwa sababu huduma mbalimbali zinatolewa katika kituo hicho na wanafanya kazi kwa masaa24,
"kuna baadhi ya vituo vya afya gharama zinakua kubwa hasa kwa akina mama wanaokwenda kujifungua hutozwa sh 60-70 elfu,lakini kwa Kata ya Mafiga lazima utaratibu ufuatwe"Amesema Butabile
"Wananchi wote ya mafiga tumieni kituo chenu cha afya kwa kuwa kipo karibu na nyinyi na hata wanaotoka kata jirani wanakaribishwa katika kituo chetu na gharama sio kubwa na tayari tumepata jenereta kubwa la kisasa na umeme ukikata hakuna shida lazima huduma ziendelee kutolewa"Ameongeza Mhe. Butabile.
Mbali na hayo Butabile amempongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayo ifanya ya kuboresha huduma za afya nchini hususani Manispaa ya Morogoro kwani Kituo cha Afya Mafiga kipo kwenye mpango wa bajeti mwaka wa fedha 2023/2024 kwa ajili ya umaliziaji wa chumba cha upasuaji.
Sambamba na hayo Butabile amewapongeza wananchi wote kwa kuhudhuria mkutano na kuwaomba ushirikiano ili kuhakikisha wanaleta maendeleo kwenye kata yao.
Post a Comment